Magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya ngono


Magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya ngono (STDs) ni jamii ya magonjwa ambayo huathiri watu wengi hasa vijana. Magonjwa haya husambazwa hasa kwa njia ya kufanya ngono isiyo salama.

Pia huweza kusambazwa kwa kuchangia sindano, kwa mama kwenda kwa mtoto kipindi cha kujifungua, na kwa kuongezewa damu isiyo salama.

Mfano wa magonjwa haya ni kama; clamidia, homa ya ini, gonorea, pangusa na hata UKIMWI .

Kulingana na takwimu za shirika la Afya duniani. Takribani watu milion moja hupata maambukizi haya kila siku. Huku waathirika wengi wakiwa kati ya miaka 15-24.

Dalili za jumla za magonjwa haya hujumuisha:

 • kutokwa na usaha/utete-ute sehemu katika sehemu zako za siri
 • kupata kipele ambacho huenda kuwa kidonda ambacho huweza kuwa na maumivu au mda mwingine bila maumivu sehemu za siri
 • Kuwa na homa isiyo kali
 • maumivu wakati wa kukojoa

Jambo muhimu la kujua ni kuwa kwa kuangalia sehemu za siri pekee huwezi jua kwa uhakika kuwa mwezi wako ameambukizwa au la. Kwani kuna baadhi ya magonjwa haya huweza kukaa kwa jinsia flani kwa mda mrefu bila kujionyesha. Hivyo ni muhimu sana kujikinga.

Njia za kujikinga na magonjwa haya ni mojawapo na:

 • kutofanya ngono. Hii ni njia kuu na yenye mafanikio makubwa
 • Kuwa mwaminifu kwa mpenzi mmoja. Kuwa na mpenzi mmoja ambaye hana haya magonjwa ya ngono.
 • Kutumia kinga. Kuhakikisha unashiriki ngono salama kwa kutumia kinga kila unapokutana na mwezi wako.
 • Kupata chanjo. Kuna baadhi ya magonjwa haya yana chanjo. Kama homa ya ini-B na virusi vipelekeavyo saratani ya shingo ya kizazi (HPV)
 • Kupima. Kabla ya kuanza kukutana na mpenzi wako mpya, ni vyema kila mmoja akaenda kupima na kuhakikisha yupo salama.
 • Elimu. Kama mzazi muelimishe mwanao kuhusu ngono salama. Na pia ongea na marafiki zako na wadogo zako kuhusu namna ya kujikinga. Pia, ongea na mwenzi wako kuhusiana na magonjwa haya na umuhimu wa kuwa waaminifu
 • Kunywa kilevi(pombe) kwa kiasi. Takwimu zinaonesha kuwa watu wengi hupata maambukizi haya hasa baada ya kunywa pombe na kulewa na kisha huwa katika hali ya hatari ya kujihusisha na ngono isiyo salama.

Jambo la muhimu kujua ni kuwa, njia moja pekee si thabiti kuepukana na magonjwa haya. Hivyo, ni nyema kutumia njia zaidi ya moja ili kuwa katika usalama zaidi.

“Jikinge, shiriki ngono salama, tumia kinga”

3 thoughts on “Magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya ngono

  1. Wagonjwa wa autoimmune disease (ugonjwa ambao selikinga za mwili hujishambulia zenyewe) hutibiwa kwa dawa zinazoshusha kinga ya mwili (immunosuppresive drugs).. Hizi zinapotumiwa kwa muda mrefu hudhoofisha kinga ya mwili na kumfanya mtu awe na upungufu wa kinga mwilini kama walivyo wagonjwa wa ukimwi. Tofauti ni kwamba watu hawa hawana maambukizi ya virusi vya ukimwi na hawatumii ARV’s.. Kinga ya mwili inawezakushushwa pia na magonjwa kama kisukari (diabetes) kwa sababu sukari nyingi kwenye tissue za mwili huzuia ufanyaji kazi wa seli-kinga za mwili,. Kwa ujumla watu wenye upungufu wa kinga huweza kushambuliwa na maambukizi yoyote yale

 1. Nahisi uchungu mila ninapo kojoa na kuna vijipande vya damu
  Siwezi kuzuiya mkojo kwa mda hata wa dakika mbili
  Hii yaweza kuwa dalili ya nini na tibaya yake ni gani.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show