Uzito na unene uliopitiliza kwa mtoto(obesity)

Tatizo la unene na uzito uliopitiliza kwa watoto (obesity) ni tatizo ambalo linaendelea kukua katika nchi zote zilizoendelea na pia zinazoendela. Kwa mujibu wa shirika la afya duniani (WHO) takribani milioni 41 ya watoto walio chini ya miaka mitano dunia nzima wameathirika na tatizo hilo. Katika bara la Afrika tatizo limekua likiongezeka kwa asilimia 50 tangu mwaka 2000

Hii inaweza kuelezewa na sababu kama ukuaji wa teknologia na utandawazi ambayo imepelekea watu kuishi Maisha ya kutoushughulisha sana mwili, kuwepo wa vyakula ambavyo sio salama kwa afya ya binadamu

Nitajuaje kama mwanangu ana uzito na unene uliopitiliza?

Ni vigumu kugundua kwa kuangalia kwa macho kujua kama mtoto ana uzito na unene uliopitiliza. Njia rahisi ni kuhudhuria kliniki ili kujua uzito na urefu wa mtoto. Kipimo ambacho hutumila ni cha BMI ambacho hulinganisha uzito na kimo cha mtoto kwa kuchukua uzito katika kilogramu na kugawanywa kwa kipeo cha pili cha kimo cha mtoto. Kipimo  hiki hakitumiki kwa watoto walio na umri wa chini ya miaka miwili kwa sababu ongezeko la uzito hutofautiana kati ya mtoto na mtoto. Njia nyingine ni pale uzito wa mtoto utakapoongezeka kwa Zaidi ya asilimia 20% ya mategemeo ya uzito wa kawaida ya mtoto kwa wakati huo.

Nini chanzo na sababu hatarishi zinazoweza pelekea tatizo hilo?

 • Kurithi. Hii ni sababu ya kigenetiki ambapo mzazi mwenye uzito na unene wa kupitiliza ana uwezekano mkubwa wa kuzaa mtoto mwenye tatizo hilo kuliko mama ambaye hana tatizo hilo
 • Mtoto aliyezaliwa kwa mama mwenye kisukari wakati wa ujauzito
 • Dawa kama insulin, phenelzine, amitryptine, risperidone, clozapine
 • Mgonjwa kama kansa kwenye ubongo na matatizo ya homoni kwenye mwili
 • Kumwanzishia mtoto chakula mapema kabla ya miezi sita au maziwa ya kutengeneza (fomula milk)
 • Kumpa mtoto vyakula vyenye mafuta na sukari kwa wingi kama chocolate, pipi, soseji, biskuti, chipsi
 • Mtoto kukaa mda mrefu bila kucheza na wenzake, kuangalia televisheni kwa mda mrefu au kucheza na kujichangamsha.

Nini madhara kwa mtoto mwenye uzito na unene uliopitiliza?

 • .Mtoto ana hatari ya kuwa na tatizo hilo ukubwani
 • .Mtoto yupo katika hatari ya kupata kisukari, shinikizo la damu, magonjwa ya figo na moyo, kiharusi katika Maisha yake ya baadae
 • . Mtoto pia anaweza kuzomewa na wenzake shuleni kutokana na muonekano wake na hivi kumfanya mtoto asiweze kujiamini na kusoma vizuri

Nini cha kufanya ili kumkinga mtoto na tatizo hilo?

 • Kumnyonyesha mtoto kwa wingi katika miezi sita ya mwanzo
 • Kumpa mtoto chakula sahihi baada ya miezi sita kama matunda, mboga za majani, kunde, karanga, na nafaka kwa wingi
 • Kutomlisha mtoto kiasi kikubwa cha chakula. Jua mtoto akishiba na akisikia njaa ili kuepuka kumpa vhakula kingi
 • Kupunguza vyakula visivyo salama kama vikizidi mfano soseji, chipsi, pipi, soda,
 • Kwa mtoto mwenye umri wa kutembea ni vizuri akijichanganya na wenzake katoka michezo
 • Wazazi pia wawe mfano kwa watoto kwa kupunguza kula vyakula vyenye mafuta kwa wingi wakiwa nyumbani na kueouka kula vyakula kama chipsi mbele ya watoto

Ikumbukwe kuwa mtoto mwenye tatizo hili haishauriwi kumnyima chakula kama wakubwa wengi wanavyofanya (diet) bali kumpa chakula kilicho sahihi kam ilivyoelezwa hapo juu.

Usisite kumwona daktari ikiwa mtoto anaendelea kuongezeka uzito hata baada ya kumpa chakula kinachostahili.

2 thoughts on “Uzito na unene uliopitiliza kwa mtoto(obesity)

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show