Fahamu kuhusu Kwashiorkor

Huu ni ugonjwa unaosababishwa na upungufu wa protini mwilini.Kuna magonjwa mengi ya utapiamlo na kwashiokor ni moja wapo

Magonjwa haya hupata watoto kwa ujumla na haswa wale walio chini ya miaka mitano

Dalili zake ni zipi?
1)Kushindwa kukua kwa mtoto kulingana na umri wake(Failure to thrive)
2)Kukonda kupita kiasi
3)Tumbo kujaa kupita kiasi na miguu kuvimba
4)Nywele kunyonyoka na kubadilika rangi (kama dhahabu)
5)Mabadiliko ya ngozi,huwa kama inabanduka na kuwa na vidonda
6)Mtoto huchoka haraka na kukasirika kirahisi
7)Mtoto kuugua mara kwa mara kutokana na kushuka kwa kinga ya mwili

Nini cha kufanya?
Kuwahi kituo cha afya kupata vipimo(kama vya mkojo na damu) vitakavyohakiki kuwa ni kweli mtoto ana upungufu wa protini mwilini

Matibabu
Kikubwa ni kumpa mtoto vyakula vya kuongeza nguvu na protini kwenye mwili wa mtoto,pia kutumia virutubisho vyenye protini ili kupunguza dalili na ukali wa ugonjwa

Vyakula vinavyoongeza protini ni kama;Nyama,samaki,maziwa,maharage,njegere,jibini,mayai,karanga n.k

Daktari atakuelewesha namna ya kula na ratiba ya kula ili mtoto apate nafuu haraka iwezekanavyo hivyo kuna umuhimu mkubwa wa kuwahi kituo cha afya

Kama tiba itapatikana mapema mtoto anaweza akaendelea na maisha yake na ukuaji ukarejea kama kawaida

Lakini kuna uwezekano mkubwa wa mtoto kupata shida ya ukuaji wa mwili na akili kama tiba itacheleweshwa,madhara mengine ni makubwa hata kupelekea kupoteza maisha

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show