Kudumaa kwa mtoto (stunting)

Kudumaa ni hali ambapo mtoto huwa na kimo kifupi kisichoambatana na umri wake.Mtoto akipitisha umri wa miaka miwili akiwa amedumaa hali hii haiwezi kurekebishwa ama kutibiwa.

Sababu za kudumaa.

  • Kukosa lishe bora kwa watoto wachanga.
  • Magonjwa ya mara kwa mara kama kuendesha na minyoo-humfanya mtoto kupoteza madini na vitamini muhimu zinazohitajika katika kukua kwake.
  • Mama mjamzito kukosa lishe bora hueka mtoto wake katika hatari ya kudumaa pindi atakapozaliwa.
  • Uhaba wa maji safi na hali duni ya usafi wa kimwili na kimazingira huchangia watoto kuambukizwa magonjwa yanayoweza kudhuru kukua kwao.

Athari za kudumaa kwa afya na maisha ya mtoto.

  • Kimo kifupi kuliko kawaida-jambo hili linaweza fanya mtoto kukejeliwa na wenzake.
  • Kutokua kwa kiakili na kifikira-mtoto akidumaa akili yake haikui ipasavyo jambo ambalo humfanya kutatizika kimasomo na baadaye katika ajira akiwa mtu mzima.
  • Kudumaa humueka mtoto katika hatari ya kupata magonjwa sugu katika siku zake za usoni.Magonjwa haya ni kama kisukari,shinikizo la damu na kunenepa kupita kiasi.Kudumaa pia imehusishwa na vifo vya mapema.
  • Kudumaa katika watoto wa kike kunawezasababisha matatizo baadaye maishani wakati wa kujifungua kwani kiuno kitakua kidogo kuliko kawaida.Vilevile,mwanamke aliyedumaa ako katika hatari ya kujifungua mtoto aliye na uzani mdogo kuliko kawaida.Kwa njia hii kudumaa inawezapitishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine( the intergenerational cycle of malnutrition)

 

Mbinu na mikakati ya kuzuia kudumaa.

  • Kudumisha lishe bora kwa kina mama wajawazito na wanaonyonyesha na pia kwa watoto wachanga.
  • Kuhakikisha kuwepo kwa maji safi na kudumisha usafi wa kimwili na kimazingira kwa njia kama vile kutumia vyoo kwenda haja na kuosha mikono inapohitajika.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show