Fahamu kwa kina juu ya asthma

Asthma sio hali ngeni katika jamii yetu, huu ni ugonjwa unaosababishwa na kubana kwa njia ya upumuaji (Respiratory tract) pale njia hizi zinapokutana na vichochezi na njia hizi hutoa kimiminika kizito(mucus). Asthma inaweza kuwa tatizo la kawaida ila kwa wengine linaweza kuwa tatizo kubwa linalohitaji msaada wa haraka.

DALILI ZIFUATAZO NI VIASHIRIA KUWA HALI YA MGONJWA WA ASTHMA NI HATARISHI

1. Kutumia vilainisha njia (bronchodilators) mara kwa mara
2. Kupata shida kwenye upumuaji mara nyingi
3. Kupata dalili za asthma mara nyingi zinazokufanya ushindwe kuendelea na shughuli zako za kila siku

DALILI ZIFUATAZO NI VIASHIRIA VYA ASTHMA;

1. Kukohoa bila makohozi kwa zaidi ya wiki 2
2. Kutoa sauti kama filimbi mtu akiwa amelala(whistling)
3. Kukoroma(wheezing)
4. Kifua kubana
5. Kukosa usingizi kwa sababu ya hisia ya kukosa hewa

VICHOCHEZI VINAVOSABABISHA ASTHMA NI;

1. Maambukizi katika njia ya hewa kama mafua
2. Shughuli nzito (Physical activity)
3. Hewa ya baridi
4. Dawa kama vile aspirini, ibuprofen, beta blockers
5. Manyoya ya wadudu
6. Vichafuzi hewa kama vile moshi
7. Poleni za mimea
8. Hisia kali na shinikizo (stress)
9. Sulfites na vihifadhi chakula vinavotumika katika bia, matunda yaliyokaushwa na mvinyo

NANI YUPO KATIKA HATARI YA KUPATA ASTHMA?;

 • 1. Mwenye ndugu alie na asthma
  2. Watumiaji wa sigara
  3. Wanaokaa karibu na wavuta sigara (second hand smokers)
  4. Uzito uliopitiliza
  5. Wanaofanya kazi katika viwanda vyenye uchafuzi wa hali ya hewa kama vile migodi
 • NIFANYE NINI NIKIGUNDULIKA NINA ASTHMA?; 
 •  1. Ni vema kujiepusha na vichochezi vya Asthma                2. Tambua na tumia dawa mapema unapoisi shambulio la asthma                                             3. Fata dozi uliyopewa na mtaalamu wa afya.                           4. Fuatilia kwa makini mwenendo wako wa upumuaji
 • Asthma haina tiba ila kuna dawa mahususi kwa ajili ya dalili za ugonjwa huu. USITUMIE DAWA BILA KUMUONA MTAALAMU WA AFYA. Mfano wa dawa hizo ni Salbutamol na Montelukast

2 thoughts on “Fahamu kwa kina juu ya asthma

 1. Kwenye vichochezi vya asthma mojawapo ni manyoya ya wanyama kama vile paka na hata manukato(body spray) pia zinaweza sababisha chemical irritation(uchochezi wa kikemikali) ndani ya njia za hewa na kuleta mbano wa njia ya upumuaji kwa hiyo ni vema kukaa mbali na vitu kama hivo

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show