Ijue presha ya mapafu (pulmonary hypertension) na dalili zake.

Presha ya mapafu ni nini?
Hii ni presha iliyo juu ambayo huathiri mishipa ya damu iliyopo kwenye mapafu na upande wa kulia wa moyo. Hii huweza sababishwa na matatizo mbali mbali ya moyo na mapafu.

Dalili zake ni zipi?
Katika hatua za mwanzo za presha ya mapafu mara nyingi hua haina dalili lakini hujitokeza baada ya muda na hali huendelea kuwa mbaya kwa kadiri muda unavyoongezeka.
Dalili zake ni kama;
– Kupumua kwa shida. Mwanzoni hutokea ukifanya mazoezi lakini baada ya muda hujitokeza hata bila kufanya shughuli yoyote.
– Maumivu ya kifua
– Kusikia mapigo ya moyo.
– Uchovu usio na sababu maalum.
– Kizunguzungu.
– Kuvimba miguu, na tumbo.
– Mdomo wa nje (lips) na ngozi kuwa na rangi ya blue.
– Pia kama presha ya mapafu haitadhibitiwa mapema mgonjwa anaweza kukohoa damu.

Mara nyingi hili tatizo huweza kuingiliana na matatizo mengine ya moyo hivyo endapo utapata dalili tajwa hapo juu ni vema kufika katika kituo cha afya kwa vipimo na matibabu zaidi.
Ili kuzuia presha ya moyo isilete madhara zaidi, inaushauriwa kufanya mabadiliko katika maisha ya kila siku, mabadiliko hayo ni kama vile kuacha kutumia sigara, kupunguza matumizi ya chumvi na kula mlo kamili.

4 thoughts on “Ijue presha ya mapafu (pulmonary hypertension) na dalili zake.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show