Vijue vimiminika vitano viwezavyo kuhifadhi jino zima lililo chomoka ili liweze kupandikizwa tena hosipitali.

 • kuchomoka kwa jino au meno kutoka katika mfupa wa taya na kuacha pengo kitaalamu huitwa Tooth avulsion. Tafiti za kisayansi zimeonesha kuwa tatizo hili hutokea sana kwa watoto kati ya umri wa miaka 7 mpaka 14, Na meno ya mbele ya Taya la juu ndio huchomoka zaidi ukilinganisha na Taya la chini au meno ya nyuma (magego).
 • Sababu kubwa inayopelekea kutoka kwa jino la utu uzima kwa watoto wa umri tajwa hapo juu ni michezo shuleni, michezo katika viwanja vya mpira na michezo ya watoto nyumbani. Vilevile kwa watu wazima pia ajali katika maeneo mbalimbali huweza pelekea jino kuchomoka nje ya mfupa wa taya.
 • Matibabu ya kulipandikiza jino zima lililo chomoka na kuacha pengo yanawezekana kama mgonjwa atawahi kufika hosipitali ndani ya dakika tano’ hii husaidia tishu na seli za jino sizikauke na kushambuliwa na bakiteria ambao wanaweza sababisha kutofanikiwa kwa matibabu.
 • Kama mgonjwa hawezifika katika hosipitali ndani ya dakika tano basi matibabu ya kulipandikiza jino yatakuwa na matokeo mazuri kama jino litahifadhiwa vyema katika vimiminika vifuatavyo ndani ya nusu saa hata saa moja kabla ya kumuona daktari wa afya ya kinywa na meno.
  1.Maziwa freshi, ni kimiminika kilicho la virutubisho viwezavyo hifadhi seli hali za jino.
  2.Mate ya Mgonjwa, mgonjwa ateme mate ndani ya chombo kidogo kisha ahifadhi jino lake humo liwe katika mazingira yake ya kinywani.
  3. Hanks Balanced Salt solution to (HBSS) hiki pia ni kimiminika chenye chumvi hupatakina katika maduka muhimu.
  4.Saline solution, hiki pia ni kimiminika chumvi hupatikana katika duka la dawa wengi hupenda kuita maji ya dripu.
  5.Maji ya kawaida, haya hutumika tu pale ambapo uwezekano wa kupata vimiminika vyote hivyo juu imeshindikana. Maji ya kawaida kwa sababu za kisayansi si mazuri kuhifadhi seli hali za jino na huweza pelekea kufa kwa seli hai za jino.

Mgonjwa akihifadhi Jino au Meno yake ambayo yalikua ni mazima kabisa ila kwasababu ya ajali yamechomoka, Basi upo uwezekano mkubwa wa jino kupandikizwa tena punde afikapo hosipitali. Maelekezo mengine atapatiwa wakati matibabu yakiendelea.

12 thoughts on “Vijue vimiminika vitano viwezavyo kuhifadhi jino zima lililo chomoka ili liweze kupandikizwa tena hosipitali.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show