Fahamu sababu zinazosababisha kupoteza uwezo wa kusikia na matibabu yake

Kupoteza uwezo wa kusikia hutokea kama mtu hawezi kusikia kiwango cha chini cha sauti ambacho mtu anaweza kusikia (threshold).

Uwezo wa masikio kufanya kazi ya kusikia hupotea kutokana na sababu mbalimbali. Uwezo wa kutokusikia upo wa aina zifuatazo;

 • Kutokusikia kutokana na masikio kutokupitisha mawimbi ya sauti viuri
 • Kutokusikia kutokana na kushindwa kubadilisha mawimbi ya sauti kwenda katika mfumo wa umeme
 • Mchanganyiko wa kutokupitisha mawimbi ya sauti na kutokubadilisha mawimbi ya sauti kwenda katika mfumo wa umeme

Sababu zinazopelekea kupoteza uwezo wa kusikia

Sababu zinazosababisha kupoteza uwezo wa kusikia zimegawanyika katika makundi mawili katika nyanja zote mbili yaani kupitisha mawimbi ya sauti vizuri na kubadilisha mawimbi ya sauti kuwa kuwa katika mfumo wa umeme, nazo ni;

 • Sababu za kuzaliwa nazo
 • Sababu za baada ya kuzaliwa

Kupoteza uwezo wa kupitisha mawimbi ya sauti

 • Sababu za kuzaliwa nazo

-Kuzaliwa na mfereji wa kupitisha mawimbi ya sauti ulioziba au mwembamba

-Kuzaliwa na sikio la katikati lililoziba

-Kukosekana kwa ‘ossicle’ moja ya sikio au ‘ossicles’ kuungana

 • Sababu za baada ya kuzaliwa

-Nta za sikio kuwa nyingi mpaka sikio kuziba (Cerumen impaction)

-Sikio la kati kujaa maji au usaha

-Maambukizi katika sikio la nje na katikati

-Kujeruhiwa kwa sikio kwa mfano kupigwa kofi au mlipuko inaweza kusababisha ngoma ya sikio kupasuka, pia kuvunjika kwa baadhi ya mifupa inayozunguka sikio inaweza kuharibu mpangilio wa ‘ossicles’ hivyo kupelekea kupoteza uwezo wa kusikia.

-Magonjwa yanayopelekea ngoma ya sikio kuwa ngumu kama vile ‘otosclerosis’

Kupoteza uwezo wa kubadilisha mawimbi ya sauti kuwa katika mfumo wa umeme

 • Sababu za kuzaliwa nazo

-Kurithi kutoka kwa wazazi

-Maambukizi ya virusi vya Rubella

-Ugonjwa wa manjano wa mtoto mchanga

 • Sababu za baada ya kuzaliwa

-Maambukuzi kama vile matumbwitumbwi(mumps), tetekuwanga

-Ajali

-Uvimbe

-Dawa kama vile za kundi la aminoglycosides (Gentamycin,Streptomycin, Knamycin), Diuretics like furosemide and ethacrinic acid na dawa za malaria kama quinine

-Kuwa katika mazingira ya sauti kubwa kwa muda mrefu

Matibabu ya kutokusikia au kupungua uwezo wa kusikia hutegemea na aina ya tatizo.

 • Kama sababu ni ya kusafirisha mawimbi ya sauti matibabu huwa ni kulingana na sababu kama vile

-kutoa nta,kurekebisha ngoma ya sikio kama imepasuka,kurekebisha stapes kama zimekuwa ngumu, upasuaji kwa ajili ya kutoa uvimbe, dawa za kuzibua pua (nasal decongestants)

 • Kama sababu ni ya kushindwa kubadilisha sauti kuwa katika mfumo wa umeme, hakuna matibabu ila kuna vifaa vya kusaidia kusikia na kuwekewa koklea nyingine.

Kwa kufanya yafuatayo inasaidia kujikinga dhidi ya matatizo ya kusikia

-Chanjo dhidi ya Rubella

-Ushauri wa kijenetikia, kwa mfano kutokuoana ndugu wa karibu wenye tatizo la kusikia

-Kueuka matumizi ya kuzidi  ya dawa zinazoathiri masikio

Bila kusahau kutafuta msaada kiafya pale unapohisi kuna tatizo la sikio ili kutatua sababu inayoleta shida kabla ya sababu hiyo kuwa sugu na kupelekea kupoteza uwezo wa kusikia.

2 thoughts on “Fahamu sababu zinazosababisha kupoteza uwezo wa kusikia na matibabu yake

 1. Asante doctor kwa maelezo yako mazuri…. Ningëpenda kujua kama Kuna tafiti Yoyote iliyofanyika ambayo inaonyesha Kuwa matumizi ya Ear phone yanaweza sababisha matatizo ya kusikia

  1. Asante sana Chalo kwa kufuatilia na kujipatia elimu kupitia daktari mkononi.

   Si kwamba kila atakayetumia earphone anapata matatizo ya kusikia, ila ni kwamba matumizi ya earphone kwa muda mrefu na kwa sauti ya juu sana inapelekea kujeruhiwa kwa ogani za sikio na pia inasababisha kuhama kwa kile kiwango cha kawaida cha mwanadamu cha kusikia na kujikuta anazoea sauti kubwa (Hearing threshold shift).

   Pia sauti ya juu husababisha kujikaza na kubana kwa mishipa ya damu ya koklea ‘vasospasms’ na kupelekea kukosekana kwa oksijeni na kusababisha matatizo katika kusikia.

   Karibu upitie hii post pia kwa maelezo zaidi ya earphones http://daktarimkononi.com/?s=earphone

   Uliuliza kuhusu researches pia, vitabu vya afya ya kama vile Maqbook na hata pages mashuhuri za afya kama vile Medscape,webMD na nyinginezo vinaeleza na wanaeleza researches zimefanyika.

   Karibu tena kama una swali

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show