Asali ni chakula na dawa

Asali ni kimiminika kitokanacho na nyuki. Nyuki hawa hutengeneza asali kwa kupita katika mimea mbalimbali, hivyo kuifanya asali iwe ni kimiminika chenye virutubisho vingi. Kwa utamu wake tunaitumia kama chakula, pia vitu vilivyomo ndani yake huifanya asali kua dawa.

Faida za asali;

1. Huponya vidonda
Haswa kwa watu walio ungua moto, asali husaidia vidonda kupona haraka. Hii ni kwasababu asali ina vitu vinavyoweza kuua vijidudu vinavyo sababisha magonjwa(bakteria).

2. Husaidia kupunguza au kuponesha kabisa kikohozi.
Mtu akiwa anakohoa, anaweza kulamba asali kijiko kimoja kama dawa kila siku na kutuliza kikohozi hicho.

3. Husaidia kupunguza uwezekano wa kupata vidonda vya tumbo na magonjwa mengine ya tumbo.
Asali ina virutubisho ambavyo huweza kupambana na bakteria( H. Pylori) ambao husababisha vidonda vya tumbo. Hivyo mtu mwenye vidonda vya tumbo anaweza kua analamba asali angalau kijiko kimoja kila siku, au kuitumia kama chakula.

4. Inaongeza nishati mwilini

Asali inasukari ambayo ikibadilishwa na vimeng’enya vya chakula mwilini hutumika kutengeneza nishati ya mwili. Sukari yake ipo sawa na ile inayopatikana kwenye vyakula vingine. Tena kiasi kidogo tu cha asali kina sukari nyingi sana ambayo yaweza kumpatia mtu nguvu hata kama hajala chakula cha kutosha.

5. Hutumika kutibu magonjwa ya ngozi na kulainisha ngozi ambayo haina ugonjwa kuifanya iwe na muonekano mzuri zaidi.

6. Huimarisha na kuboresha mfumo wa usagaji wa chakula tumboni, hivyo utaondokana na ukosefu wa choo au kutopata choo kigumu kinacho sababisha maumivu wakati wa kujisaidia.

7.Husaidia kupunguza uwezekano wa kupata saratani

8. Husaidia kuimarisha kinga ya mwili.

Pamoja na hayo yote asali yaweza kutumika na mdalasini na mimea mingine kutengeneza dawa mbalimbali. Asali imekua ikitumika kama dawa tangu enzi za mababu zetu na bado ni dawa na chakula. Kiafya waweza kua unatumia asali kuweka kwenye chai badala ya sukari, kupaka kwenye mkate au kulamba. Hii itasaidia kupata faida zote za asali kwenye mwili wako.

5 thoughts on “Asali ni chakula na dawa

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show