Kula kupita kiasi (Overeating)

Tamaduni hasa kutoka nchi za nje zimetuzoesha kuwa na utaratibu wa kuleta chakula mezani kwa awamu. Mara nyingi huwa na awamu tatu; kianzishi / kishtua tumbo (starter), mlo wenyewe (main course) na kisindikizaji (dessert).

Bila kujua mlo unaofuata baadaye, mtu aweza kushiba chakula kilichopo kwa wakati huo, ambacho mara nyingi huwa hakijitoshelezi kukidhi mahitaji ya mwili. Mlo mwingine unapoletwa, hulazimika kuvuka mipaka na kuchukua tena walau kidogo ili mradi aonje kila kilichopo mezani. Hii huathiri mfumo mzima wa mmeng’enyo wa mwili. Ni vyema zaidi kama vyakula vyote katika mlo husika viwekwe mezani kwa pamoja kutoka mwanzo, ili kumpa nafasi mtu aweze kuchagua chakula bora kinachomfaa kwa kiwango stahiki.

Mara nyingi, madhara ya kula kupita kiasi huonekana papo kwa hapo. Mara zingine, hakuna kuhisi maumivu, lakini viungo vinavyohusika na mmeng’enyo wa chakula hupoteza nguvu zake za asili na kuweka msingi wa kudumaza nguvu za mwili.

Chakula hicho cha ziada hupelekea kuongezeka kwa damu tumboni kupita kiasi, hivyo kusababisha mikono na miguu (extremities) kupata baridi kwa haraka zaidi. Huweka mzigo mkubwa sana juu ya viungo vya mmeng’enyo wa chakula na baada ya viungo hivi kumaliza kazi yake, kuna hali ya uchovu wa mwili. Baadhi ambao huwa na tabia ya kula kupita kiasi hudhani kuwa hali hii ni njaa lakini kiuhalisia sababu kuu ni ufanyishwaji kazi uliopitiliza wa viungo vya mmeng’enyo wa chakula. Pia virutubisho vya ziada vinavyobaki, hasa mafutamafuta hutunzwa mwilini na huweza kupelekea kunenepa.

Dalili zote hizi hutokea kwa kuwa asili ya mwili hukamilisha kazi yake kwa kutumia nguvu kubwa isiyo ya lazima, hivyo huchoka sana. Tumbo mara nyingi husema “Nipumzishe”. Lakini kwa wengi, uchovu huu hutafsiriwa kama hitaji la chakula zaidi hivyo mzigo mwingine mkubwa huwekwa juu ya tumbo. Viungo vya mwili hudhoofika kwa kufanyishwa kazi kupita kiasi wakati ambapo vingeweza kukamilisha kazi yake kwa namna isiyoleta athari mwilini.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show