Kuna faida ya kula matango?

Matango ni matunda ambayo yanafaida kubwa katika mwili wa binadamu lakini cha kwanza kabisa,

Je, unafahamu jinsi ya kula matango kwa usahihi?

Kumenya tango ili kuondoa maganda kunaharibu virutubisho vilivyo ndani ya tango, hivyo unapoandaa matango usiyamenye. Yasafishe vizuri kwa maji safi yaliyochemsha kisha kula tango pamoja na maganda yake, kwa kufanya hivi utakua umepata virutubisho vingi.

Matango yanafaida gani?

1. Husaidia ubongo kufanya kazi vizuri
Hulinda mishipa ya fahamu na neva katika ubongo. Hupunguza kasi ya kusahau kipindi mtu anapozeeka ambako hutokana na ugonjwa unaoitwa Alzheimer’s, matango husaidia kutunza kumbukumbu.

2. Hupunguza vihatarishi vya saratani
Kwa saratani za matiti, mfuko wa uzazi, ova na tezi dume. Matango husaidia kupunguza kasi ya ukuaji wake,kwani matango huwa yana Virutubisho viitwavyo lignans ambavyo hupunguza hatari ya mtu kupata saratani hizi.

3. Kupunguza uvimbe
Matango hupoza uvimbe kwa kuzuia baadhi ya vichocheo vya mwili kutengeneza uvimbe huo.

4: Huepusha harufu mbaya mdomoni.
Kwa kuweka kipande kidogao cha tango mdomoni husaidia kuondoa harufu mbaya ya mdomo. Kata kipande kidogo cha tango na liweke juu ya ulimi baki nalo kwa dakika tano, kisha unaweza ukalitoa au ukalitafuna na kulimeza. Pia unaweza kula matango kwa wingi na ukaepuka harufu mbaya

6. Kupunguza msongo wa mawazo.
Matango yana uwezo wa kukuondolea msongo wa mawazo na hofu katika mwili. Matango yana vitamini B ambayo husifika katika kuondoa hali hizi.

7.Matango husaidia katika mmeng’enyo wa chakula
Ni vema kama ukitumia matango kusaidia katika kumeng’enya chakula, husaidia katika ufonzwaji wa chakula pamoja na kulainisha choo.

8.Pia matango huimarisha na kuing’arisha ngozi. Ifuatayo ni njia ambayo unaweza ukatumia matango katika kutunza ngozi yako.

Tengeneza mchanganyiko wa tango na parachichi, mchanganyiko huu unatengenezwa kwa kutumia;

Tango nusu
Parachichi nusu
Sehemu ya yai isiyo na kiini
Maziwa nusu kikombe

Changanya Mchanganyiko huu vizuri, ukishalainika paka usoni na subiria kwa dakika kumi kisha nawa uso. Ukirudia zoezi hili walau mara moja kwa wiki itaimarisha ngozi na kuifanya nyororo.

6 thoughts on “Kuna faida ya kula matango?

  1. Kazi nzuri daktarimkononi,,je matango ukichanganya na vitu vingine kama kwenye kachumbari bado unaweza kupata hizi faida au tu mpaka ulile lenyewe?

  2. Asante dokta naomba kuuliza swali,,je ni sahihi kula matango na chumvi au tule makavumakavu tu? Je kuna hatari ya kuweka chumvi?

    1. Asante kwa swali zuri Merdald
      Tunaongeza chumvi kwa ajili ya ladha, ila si vyema kula tango na chumvi ni vizuri zaidi ukila bila chumvi. Pia chumvi ya kuongeza juu ya chakula au tunda inamadhara kiafya. Chumvi inabidi iwe imechanganyika na chakula kilicho pikwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show