Matumizi ya pamba za usafi (pedi)

Pedi huvaliwa kama nepi za watoto (pampers/diaper) mwanamke akiwa katika hedhi zake ili kunyonya uchafu utokao kipindi hicho. Huwekwa kwenye nguo ya ndani ya mwanamke na hukutana na sehemu ya siri ya mwanamke moja kwa moja. Aina nyingine ya pamba hizo ambazo zinaweza kutumika ni kama tampons au menstrual cup ambayo huchomekwa kabisa ndani ya uke wa mwanamke kukusanya (kwa menstrual) cup au kufyonza (tampons) hedhi. Pale ambapo mwanamke hukosa vitu hivi na hupata dharura huwezaa kutumia karatasi ya choo (toilet paper) na kuweka juu ya nguo ya ndani.

Matumizi ya pedi.

Kumkinga mwanamke kuchafuka na hedhi anayoipata kila mwezi. Hunyonya hedhi na kumfanya mwanamke kuweza kuendelea na shughuli zake za kila siku. Hufungwa kwenye karatasi la nailoni ambalo mara nyingi hutumika kuifunga pedi kabla ya kuitupa baada ya kubadilisha. Haziruhusiwi kutupwa kwenye choo (zaidi ya choo cha shimo). Huweza kutumika pia katika huduma ya kwanza kuzuia damu kama hakuna pamba. Watu ambao hushindwa kubana mkojo pia hutumia pedik kujikinga kuchafuka.

Aina za pedi.

 1. Pedi ambazo huweza kutumikana kutupwa baada ya matumizi ya kwanza :
 • Panty liner (kwa ajili ya hedhi inayotoka kidogo au inayoishia kabisa).
 • Ultra-thin pads (nyembamba sana, kwa ajili ya wanawake wenye hedhi zinazotoka kidogo).
 • Regular (kwa hedhi inayotoka kawaida).
 • Maxi/super (kwa ajili ya hedhi zinazotoka kwa wingi na nzuri kwa siku za mwanzo).
 • Overnight (ndefu Zaidi na hutoa kinga pindi mtumiaji anapokua amejilaza).
 • Maternity (ndefu Zaidi ya maxi/super na hutengenezwa kunyonya damu itokayo baada ya kujifungua (lochia)).
 1. Pedi ambazo haiziitaji kutupwa baada ya matumizi ya kwanza

Pedi za vitambaa.

Watu wengine hutumia pedi amabzo huweza kufuliwa na kutumiwa tena hedhi ijayo. Nyingi hutengenezewa kitambaa aina ya cotton. Endapo mtu akishindwa kununua pedi, huweza kutumia kitambaa chochote aina ya koton na kukisafisha vizuri. Vitambaa vianvyouzwa huweza kua na mabawa ya kuzungushia nguo ya ndani au bila mabawa. Zilikua zikitengenzwa na mikanda yake ya kufunga. Hizi hazihitaji kutupwa hivo husaidiai wasioweza kununua pedi kila mzunguko. Haziwekewi manukato ya aina yoyote (tofauti na pedi za kutupa) na husemekana kutokuleta muwasho/harara.

Je, pedi huwa na tarehe ya mwisho ya matumizi (expiry date)?

Ukilinganisha na vyakula, pedi hazina siku ya mwisho ya matumizi. “Kama karatasi isivyoweza kuharibika, ndivo pedi isvoweza kuisha muda wake wa matumizi”, asema KOTEX.

Nivae pedi kwa muda gani?

Kwa siku ambazo hedhi hutoka nyingi, pedi yenye pamba nyingi huweza kutumika. Haijalishi hedhi hutoka kwa kiasi gani, pedi hutakiwa kubadilishwa baada ya masaa matatu au manne (3-4). Kuvaa pedi kwa muda mrefu hufanya mwanamke kutoa harufu mbaya na pia vimelea huota kutoka kwenye hedhi na kuletea magonjwa. Kama hedhi ni nzito, pedi huweza kubadilishwa kabla ya masaa hayo.

Madhara ya kuvaa pedi muda mrefu.

 • Huweza kusababisha saratani
 • Huwa na kemikali iitwayo dioxin ambayo si salama kukutana na mwili kwa muda mrefu.
 • Inaweza kusababisha ugumba au mtoto kuzaliwa na matatizo.
 • Ni mazingira rafiki kwa ukuaji wa vimelea vya bakteria hivo kusababisha maradhi mengineyo.

 

4 thoughts on “Matumizi ya pamba za usafi (pedi)

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show