Dalili za jino kutoboka

Kutoboka (kuoza)  kwa jino ni hali ya jino  kutengeneza tundu ikiwa ni matokeo ya uwepo wa mara kwa mara wa tindikali inayozalishwa na bakteria baada ya mtu kula vitu vyenye sukari. Mara nyingi watu husubiri mpaka jino litoboke na kuwa na shimo kubwa na maumivu makali ndipo waende kwa daktari wa kinywa na meno kwaajili ya matibabu.

Zifuatazo ni dalili za jino lililotoboka.

 • Katika hatua za mwanzo jino lililoathirika huwa na alama nyeupe kama ya chaki kwenye eneo lililoathirika. Alama hii ni rahisi kuonwa na daktari wa kinywa na meno anapokuchunguza hivyo ni vyema kuonwa na daktari mara kwa mara kwa ajili ya uchunguzi.
 • Jino lisipotibiwa na/au visababishi vinavyoozesha meno kuondolewa, sehemu iliyoathirika hubadilika rangi na kuwa ya kahawia (brown) au nyeusi.
 • Baada ya muda sehemu hiyo huharibika zaidi  na kutengeza tundu. Tundu likiwa dogo na katika sehemu ya juu ya jino (enamel) huwa halina maumivu.
 • Chakula hujikusanya katika tundu na kusababisha harufu mbaya pamoja na kuendelea kuongeza athari ya jino kutoboka zaidi.
 • Mara tu tundu lifikapo katika sehemu ya kati ya jino (dentine) mtu hupata dalili za maumivu hasa wakati wa kula au kunywa vyakula vya baridi au moto, vyenye sukari au asidi (tindikali ).
 • Maumivu makali ya jino yanayosababisha kukosa usingizi huweza kusababishwa na tundu kuwa kubwa na kufika katika sehemu hai ya jino (pulp chamber).

Mara uonapo dalili zozote za jino kutoboka, hata kama halina maumivu ni vyema kumuona daktari wa kinywa na meno kwa ajili ya matibabu na ushauri. Matibabu  ya tundu dogo ni rahisi kuliko tundu kubwa na lenye maumivu. Kusubiri  kwa muda mrefu bila kupata ushauri na msaada wa kitaalamu huweza husababisha madhara makubwa kama kupata jipu katika jino (odontogenic abscess) au uvimbe  katika sehemu mbalimbali za usoni (facial space infection).

Kuepuka kutoboka kwa meno, punguza ulaji wa vyakula vyenye sukari hasa katikati ya milo mikubwa (in between meals)”.

5 thoughts on “Dalili za jino kutoboka

  1. Asante. Jino linapokuwa na maumivu wakati wa kula vitu vya moto sana au baridi sana huweza kuwa ni dalili ya kutoboka.Pia huweza kusababishwa na jino kulika na kusababisha sensitivity. Ni vyema ukamuona daktari wa kinywa na meno kwa ajili vipimo zaidi.

 1. Dr asantekwa Elimu mimini mjamzito wa week 32 ninatatizo la kutoboka kwa jino gego upande wa juu na upande huondio pekee nilikuwa naweza kutafuna
  Jenaweza kuziba ktk kipindi hiki? Kasasa magego ya juu pande zote yametoboka.Asante

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show