Je, Kama mama unajua faida zikupatazo unaponyonyesha mtoto?

Imekuwa desturi kwamba wakina mama wengi hasa wafanya kazi kufanya maamuzi ya kutokunyonyesha au kunyonyesha kwa miezi michache tu.

Ukweli ambao wakina mama wengi hawaujui ni kwamba kunyonyesha sio tu kwa ajili ya afya ya mtoto wako bali pia ina faida nyingi sana kwako wewe kama mama.

Faida za kunyonyesha kwa mama ni kama zifuatazo:-

•Husaidia kupunguza mwili upatikanao wakati wa ujauzito haraka.

•Kunyonyesha hufanya mwanamama atoe homoni iitwayo oxytocini ambayo husaidia kurudisha tumbo la uzazi katika hali ya kawaida na kupunguza damu nyingi kutoka ukeni baada ya kujifungua.

•Unaponyonyesha unaongeza homoni iitwayo prolaktini ambayo huchelewesha yai kupevuka hivyo kuchelewesha uwezo wako wa kupata mimba na hivyo kuwa kama njia ya uzazi wa mpango na pia huchelewesha kuingia katika mzunguko wa hedhi.

•Ni njia nzuri ya mama kumjua vizuri mtoto na kujenga mahusiano mazuri nae.

•Hupunguza uwezo wa kupata baadhi ya saratani, mfano saratani ya ziwa. Takwimu zinaonyesha kwamba kila mwaka unaponyonyesha unapunguza uwezo wa kupata saratani kwa asilimia 4.3%.

•Ni nafuu.

•Unyonyeshaji pia hupunguza huzuni uwapatao baadhi ya wakina mama baada ya kujifungua (post partum depression).

Hakikisha:

-Unamnyonyesha mtoto kila muda anapoonyesha uhitaji na kila unyonyeshapo iwe sio chini ya dakika10 kwa masaa 24.

-Unanyonyesha kwa muda usiopungua miezi sita na mpaka mtoto afikishapo miaka miwili kwa matokeo mazuri zaidi.

Kuna faida nyingi sana za kunyonyesha mtoto kwako mwanamama, Hivyo kama mama, Jivunie kunyonyesha!

 

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show