Ectropion ya shingo ya kizazi;sababu ya maumivu wakati wa tendo la ndoa

Wanawake wengi waliopo katika umri wa kuzaa Yaani kati ya miaka(18-35)hupata mabadiliko ya shingo ya kizazi bila wao kufahamu.Mara nyingi hugundulika pale ambapo mwanamke amekwenda kumuona daktari wa wanawake kwa ajili ya sababu zingine na daktari huyo kulazimika kufanya uchunguzi wa ndani ya sehemu za siri na kukutana na hali hii (pelvic examination).
Ectropion ya shingo ya kizazi ni nini?
Ni ambapo seli laini zilizopo ndani ya shingo ya kizazi ambazo huitwa“glandular cells” kuhamia (transformation) upande wa nje wa shingo ya kizazi ambayo huwa ina seli ngumu ziitwazo “squamous epithelial cells” na kufanya shingo ya kizazi kuwa nyekundu sana na kuvimba.kwa kawaida upande wa nje wa shingo ya kizazi kuna seli ngumu (squamous epithelial cells) ambapo kukibadilika na kuwa na seli laini hupelekea kuwepo kwa dalili za hali hii.
Nini sababu ya mabadiliko haya?
Sio rahisi kugundua sababu za ectropion.Wanawake wengine huzaliwa na hali hii ya mabadiliko katika seli za shingo ya kizazi. Lakini sababu chache zinaweza kusababisha;

 • Mabadiliko ya homoni katika mwili wa mwanamke ndio maana waathirika wengi ni wasichana waliokatika umri wa kuzaa na wajawazito.
 • Utumiaji wa dawa za uzazi wa mpango ambapo husababisha mabadiliko katika homoni.
  Nini dalili?
 • Maumivu wakati wa tendo la ndoa.
 • kutokwa na damu wakati au baada ya tendo la ndoa.
 • Kupata matonematone (spotting) ya damu katikati kabla ya kufikia hedhi.
 • kutokwa  na ute mwepesi
  NB;ectropion ya shingo ya kizazi sio sababu pekee inayosababisha dalili hizi.Endapo unapata dalili kama hizi nenda kamuone daktari.

Habari  njema ni kwamba;

 • Ectropion ya shingo ya kizazi inaweza kupona yenyewe,matibabu huitajika pale ambapo dalili zimeanza na humkwaza mgonjwa.
 • Ectropion ya shingo ya kizazi sio saratani ya shingo ya kizazi havina uhusiano wowote,atakama shingo ya kizazi ya ectropion inaweza kufanana na ya saratani ikiwa bado mwanzoni yaani kubadilika rangi kuwa nyekundu sana na kuvimba.Daktari anaweza kufanya baadhi ya vipimo kuhakikisha sio saratani ya shingo ya kizazi kama vile papsmear au biopsy (kuchukua kinyama cha shingo ya kizazi na kukipima)
 • Ectropion ya shingo ya kizazi sio hali hatarishi na inapona.Daktari anaweza kuamua kufanya matibabu endapo unapata dalili semwa hapo juu na kugundua kuwa sababu ni ectropion na si vinginevyo.Anaweza kufanya  “cauterization ya shingo ya kizazi” ambapo katika mazingira yetu hutumia kifaa maalum kuziunguza seli hizo zilizotoka nje kutokea ndani. Na baada ya wiki nne mtu hupona kabisa,ambapo ndani ya hizo wiki nne daktari hushauri kutokujaamiiana na mwenza wako kupunguza hatari ya maambukizi mengine.
  Rudi hospitali endapo unapata dalili hizi;
 • Kutokwa na ute wenye harufu sana.
 • Kupata  hedhi kwa muda mrefu isivyo kawaida
 • Kutokwa  na damu nyingi sana wakati wa hedhi.
  Dalili hizi zinaweza kuashiria maambukizi baada ya matibabu;zisipuuzwe.

2 thoughts on “Ectropion ya shingo ya kizazi;sababu ya maumivu wakati wa tendo la ndoa

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show