Fangasi sehemu za siri kwa wanaume

“Fangasi sehemu za siri kwa wanaume ni moja ya matatizo sugu hasa kwa wanaume wanaoishi maeneo yenye joto.”

Kwa muda mrefu sasa kumekua na fikira ambazo si sahihi  kwamba kila unapopata muwasho  sehemu za siri chanzo chake ni maambukizi ya fangasi.

Lakini ukweli ni kwamba kuna sababu nyingi sana zinazopelekea kuwashwa  sehemu za siri,baadhi ya hizo ni pamoja na;

  • Maambukizi ya fangasi ya ngozi
  • Chawa sehemu za siri
  • Magonjwa ya upele (scarbies)
  •  Maambukizi ya bakteria

Magonjwa ya zinaa.             

Maambukizi ya fangasi sehemu za siri kwa wanaume husababishwa na fangasi aina ya  candinda albicans ambao hushambulia sana ngozi ya korodani pamoja na tinea cruris ambao hushambulia sana maeneo ya mapaja na pembezoni mwa korodani. Maambukizi haya hushamiri na kuonekana kwa mtu mwenye upungufu wa kinga mwilini, matumizi ya muda mrefu ya dawa za kuua bakteria, au mlundikano wa jasho kwa muda mrefu.

Dalili za fangasi

  1. Kuwashwa kwa muda mrefu sehemu za siri
  2. Maumivu kama ya kuwaka moto sehemu hizi hasa baada ya kujikuna kwa muda mrefu au kutumia sabuni.
  3. Kujikunja na kubabuka kwa ngozi eneo hilo.
  4. Michubuko midogomidogo inayouma sana baada ya mazoezi au kazi ya kukutoa jasho.
  5. Eneo hilo kuwa na rangi nyekundu.
  6. Michubuko kutoa maji maji yenye harufu ya uvundo.

Je matibabu ya tatizo hili ni yapi??
Tatizo hili linatibika, zipo dawa mbalimbali za poda, cream pamoja na vidonde. Ni muhimu kutembelea kituo cha afya kilicho karibu nawe kwanza kabisa ili kubaini kama ni maambukizi ya fangasi au la.. pia kupewa aina ya dawa inayokufaa.

Unaweza kufanya yafuatayo ili kupunguza maumivu kama una maambukizi haya au kupunguza hatari ya kupata maambukizi haya.
1;Oga kila baada ya kufanya mazoezi au kazi yoyote ya kutoa jasho
2;Epuka kuchangia nguo hasa za ndani  na taulo
3;Osha sehemu zako za siri kwa  maji safi ya vuguvugu pamoja na sabuni kama sehemu ya usafi wako wa kila siku
4;Kausha maji kwa kitambaa safi kwenye eneo hili baada ya kuoga
5;Badilisha nguo za ndani kila siku baada ya kuoga
6;Epuka kuvaa nguo zinazobana sana kwa sababu zinasababisha mlundikano wa jasho.

7;Tumia pia nguo za aina ya pamba zina uwezo wa kusharabu jasho na kukuacha mkavu.
8;Tumia poda maalumu inayokufanya kua mkavu muda wote eneo hilo la siri
9;Chukua hatua ya kutafuta tiba kwa maambukizi ya fangasi katika eneo lolote la mwili

1 thought on “Fangasi sehemu za siri kwa wanaume

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show