Madhara ya utumiaji wa toothpick mara kwa mara.

Toothpick ni njiti nyembamba inayotumika kuondoa mabaki ya chakula katikati ya meno.

Utumiaji wa toothpick umekuwa ni mojawapo ya njia ya kutoa mabaki ya chakula katikati ya  meno na kwakuwa ni bei nafuu na hupatikana kwa urahisi, asilimia kubwa ya watanzania hutumia njia hii.

Kuna aina mbili za toothpick

  • Aina ya kwanza ni kutokana na malighafi iliyotumika kutengeneza;kuna zilizotengenezwa kwa mbao na zingine za plastiki lakini hufanya kazi kwa usawa ule ule.

    toothpick za plastiki
  • Aina ya pili ni kutokana na umbo la toothpick kwenye ncha zake;kuna zenye ncha ya duara na zingine za pembe tatu.Zile za duara ndio ambazo zinapatikana kila sehemu na wengi wetu huzitumia.
toothpick zenye ncha ya pembe tatu

Zile zenye ncha ya pembe tatu hupatiakana mara nyingi kwenye maduka ya dawa na ndizo ambazo madaktari wa afya ya kinywa na meno hushauri zitumike kuondoa mabaki ya chakula.Hii ni kwasababu umbo la nafasi kati ya jino na jino ni ya pembe tatu na hivyo kufanya usafishaji  kuwa mrahisi na pia kuzuia kuumiza maeneo mengine ya jino na fizi.

Madhara ya kutumia toothpicks mara kwa mara ni;

  • Maumivu kwenye fizi ya meno yanayotobolewa mara kwa mara.Wakati mwingine damu pia inaweza kutoka na fizi kuvimba.
  • Toothpick inaweza kuvunjika katikati ya meno na kusababisha maumivu makali
  • Husababisha nafasi katikati ya meno kuongezeka(interdental space)

Ni kweli kwamba  huwezi kutembea na mswaki  kila mahali na mara nyingine itakulazimu kutumia toothpick hivyo unashauriwa kutembea na nyuzi safishi (dental  floss) ili kuepusha kutumia toothpick mara kwa mara.

nyuzi safishi (dental floss)

Ukitumia toothpick usilazimishe iingie katikati ya meno badala yake pitisha tu taratibu hadi mabaki yote yatakapotoka.

Usisite kumuona daktari  ukiona hali ya chakula kuganda kwenye meno imekuwa ya kujirudia mara kwa mara .

 Jitahidi kuepuka matumizi ya toothpick mara kwa mara ili kutunza afya ya meno na fizi yako na endapo utatumia basi tumia zile ambazo ncha zake zina umbo la pembe tatu.

 

2 thoughts on “Madhara ya utumiaji wa toothpick mara kwa mara.

  1. Haah kumbe unaposafisha meno saaana kwa hivyo vijiti, ndivyo nafasi kati ya meno inavozidi kuongezeka. Na ndiyo mabaki yanavyozidi kupata nafasi zaidi hivo kupelekea uhitaji wa kusafisha kuongezeka zaidi. Duu na ndivyo inavyopelekea nafasi(interdental space) kuo….. Wait, hili duara halina mwisho mzuri.
    Asante sana Dr. Fortunata

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show