Mambo ya muhimu kuhusu ugonjwa wa amoeba

Amoeba ni ugonjwa unaosababishwa na kimelea (parasite) kiitwacho Entamoeba histolytica. Ugonjwa huu huathiri sana nchi zinazoendelea, Tanzania ikiwa miongoni mwao. Na chanzo kikubwa ikiwemo mfumo wa maji kutokuwa salama.

Japokuwa mtu aliye athirika na ugonjwa huu wa amoeba anaweza asiwe na dalili, baadhi ya dalili kuu za ugonjwa huu hujumuisha:

 • kupata choo ambacho ni kilaini sana (kuharisha)
 • maumivu ya tumbo
 • tumbo kuvuta

Katika jamii watu ambao wapo kwenye uwezekano mkubwa wa kuambukizwa ugonjwa wa amoeba hujumuisha:

 • watu wanaoishi katika mazingira yasiyo na usafi madhubuti hasa usafi wa choo
 • watu wanaokaa katika vituo vyenye mazingira yasio salama kiafya kwa usafi. Mfano, magereza
 • watu ambao kinga ya mwili iko chini. Mfano, watoto wadogo, wazee, watu wenye magonjwa yanayosusha kinga ya mwili kama saratani, kisukari na maambukizi ya virusi vya UKIMWI.

Namna ambayo kwa mazingira ya kawaida ya nyumbani huweza kujizuia na ugonjwa wa amoeba inajumuisha;

 • kuosha mboga za majani vyema kwa maji masafi kabla ya kuzipika
 • Kabla ya kula tunda, osha mwenyewe na maji safi vizuri na kisha menya ganda la nje kabla ya kula au kutengenezea juisi
 • kunywa maji safi ambayo yamechemshwa na kuchunjwa vyema. Au waweza kunywa maji ya chupa mfano maji ya kilimanjaro. Lakini epuka kunywa maji yanayouzwa kwenye mifuko.
 • kunywa maziwa yaliyochemshwa vyema
 • usipendelee sana kula vyakula vinavyouzwa magengeni. Kwani vyakula vya magengeni, vingi haviandaliwi katika mazingira ya usafi thabiti. Jijengee tabia ya kuandaa chakula chako nyumbani katika hali ya usafi.
 • Usisahau kuosha mikono kwa sabuni na maji safi kila utokapo chooni.

“Jikinge, imarisha usafi wa familia yako”

2 thoughts on “Mambo ya muhimu kuhusu ugonjwa wa amoeba

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show