Vyanzo na kazi za Vitamini D kwa watoto

Vyanzo vikuu vya vitamini D ni mwanga wa jua (la jioni au asubuhi) ila tunaweza vipata kutoka kwenye vyakula pia.
Vyakula hivi mara nyingi pia huwa na uwezo mkubwa wa kutupa madini ya ziada kama ya calcium

Baadhi ya vyakula hivyo ni:-
1)vyakula vitokanavyo na maziwa mfano.jibini,maziwa fresh na hata ya mtindi
2)mbogamboga mfano.spinach ,maharage ya soya
3)samaki mfano. Aina ya Tuna na Salmon
4)nyama haswa maini
5)Mayai hasa viini vyake
6)Matunda kama parachichi,maembe

Kazi za vitamini D
1)kazi yake kuu ni kusaidia calcium kuingia mwilini na kusaidia uimarishaji wa mifupa na misuli mwilini

2)Vitamini D Ina mchango pia kwenye matibabu ya magonjwa kama maumivu ya muda mrefu(chronic pain),msongo wa mawazo,magonjwa ya moyo (kama shinikizo la damu) na hata yanayosumbua mfumo wa kinga wa mwili (Autoimmune diseases)

Mengineyo kuhusu Vitamini D

Tafiti mbalimbali zimeonesha pia kuna uhusiano mkubwa wa upungufu wa vitamin d na kansa mbalimbali kama za utumbo,titi na hata tezidume

Kuna mchango mkubwa pia unaotolewa na figo na Ini la binadamu katika kubadilisha vitamin D kuwa katika mfumo unaoweza kutumika na mwili hivyo shida za figo au ini huweza leta upungufu wa vitamini D mwilini hata kama unapata mwanga wa jua na vyakula vya kutosha

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show