Je? Nifanye nini kuepuka na bawasiri

 


Bawasiri sio ugonjwa uliozoeleka kwa watu na sio rahisi kukuta watu wakiliongelea lakini bawasiri ni ugonjwa ambao huweza kuleta aibu na wasiwasi kwa mtu azipataye na huweza pia hatarisha afya zetu pale zitakaposababisha kutokwa na damu nyingi na kupelekea magonjwa mengine kama kupungukiwa damu, maambukizi ya kwenye damu, damu kuvimbia kwenye mfumo wa choo nakadhalika

Matibabu ya bawasiri hutegemea na aina zake..

kwa bawasiri zinazotokea kwa nje dalili zinapojionesha kama uvimbe kujitokeza na maumivu unaweza nawa kwa maji moto yenye dettol au kujipaka mafuta eneo hilo kama vaseline na kunywa dawa za maumivu..

Na kwa upande wa bawasiri zilizojificha kwa ndani hizi daktari wako anaweza zitoa kwa kuzibana na baadae kukatika

Hizi njia zote huleta nafuu kwa muda ila vyaweza kurudia lakini ni muhimu kufuata njia ambazo zinasaidia kuepusha kabisa bawasiri

Zifuatazo ni njia tunazoweza tumia ili kuzuia bawasiri hasa zipo katika kubadilisha mfumo wa maisha yetu
1. Jitahidi kunywa maji ya kutosha angalau lita 1.5 mpaka 2 kwa siku
2. Pendelea kula vyakula vyenye fiber kama matunda, mboga za majani, ngano isiyokobolewa, jamii ya kunde kama maharage
3. Fanya mazoezi ya kutosha kama kukimbia na mazoezi mengine ya viungo kama yoga
4. Pendelea kutoa choo asubuhi au mara baada ya kula ambapo mfumo wa choo hufanya kazi zaidi

 

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show