MASWALI, MAJIBU NA MAONI.

Jacquilline kutoka Arusha: kuna muda jicho langu la kushoto huona nusu, shida ni nini?

Jibu: kuna sababu nyingi zinazoweza kusababisha tatizo hilo. Yawezekana ni tatizo kwenye mfumo wa macho au pia tatizo katika mfumo wa ubongo au kuumwa kichwa sana nk. Inashauriwa kumuona daktari au kituo cha huduma ya macho haraka iwezekanavyo.

Thereza kutoka Misungwi: kwanini macho yangu yanatoa machozi na kuwasha sana?

Jibu: macho kuwasha hutokana namambo kadhaa kama:

 • Kupata aleji au kuvimba (inflammation).

 • Kope kugusana na jicho au kitu kuingia jichoni.

 • Macho kuwa makavu (kutokua na machozi ya kutosha).

 • Kutumia vitu vinavyoweza kuleta muwasho kwenye macho kama manukato nk.

 • Matumizi ya lenzi za kuweka ndani ya macho (contact lens) nk.

Anisia kutoka Singida: je, kuna tatizo lolote linaloweza kutokana na kukuna macho endapo yatawasha?

Jibu: kukuna macho yanayowasha huweza kusababisha madhara zaidi kwenye jicho, huweza kusababisha jicho kuuma na kuvimba (inflammation) na kuharibu mboni ya jicho. Pia mikono yetu ina vimelea vingi, kukuna jicho hupelekea vimelea hivo kuingia jichoni na kuleta madhara mengine.

Anisia kutoka Kilimanjaro: njia mbadala ya kutatua tatizo la macho kuwasha baadala ya kuutumia dawa ni ipi?

Jibu: safisha macho yako na maji mengi, baridi na masafi au safisha na kitambaa kisafi cha maji ya baridi.

User 1 kutoka Dar: uchafu ukiingia jichoni hutolewaje?

Jibu: uchafu hutolewa kwa njia ya machozi, endapo ukiingia jichoni, mwili huutoa kwa kutoa machozi na kusafisha macho.

 

 

 

6 Comments

 1. Elina wa dodoma

  sasa dokta macho yakiingia mchanga tunavopulizaga huwa ni sahihi?

  je kuna hatari kuweka jicho kwenye maji unapoingia mchanga?!

  1. Shukran kwa kuuliza.
   Kupuliza jicho kwa ajili ya kuutoa mchanga ni sahihi kwani husaidia jicho kuutoa kiurahisi mchanga huo.
   Kuweka jicho kwenye maji hakuna shida japo unaweza sikia kama jicho kuwasha kwa kugusana na maji.
   Ni vyema ukajaribu kutoa mchanga kama unaonekana au ukawahi kituo cha afya ili utolewe bila madhara.
   Shukran na karibu daktari mkononi

  1. Shukran kwa swali
   Kumwekea mtoto maziwa jichoni kunaweza sababisha muwasho hivyo akazidi kulia
   Inashauriwa kama ameingiwa na mchanga au utomvu wa mmea machoni ulioshe jicho kwa maji mengi na masafi ili kusaidia kuondoa utomvu na mchanga.
   Kama mchanga au utomvu bado haujatoka na mtoto analia ni vyema ukawahi katika kituo cha afya kwa msaada zaidi
   Karibu daktari mkononi na shukran kwa kututembelea.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.