Dhana mbalimbali kuhusu afya ya macho

Kuna baadhi ya dhana mbali mbali katika jamii kuhusu afya ya macho hizi ni baadhi tu

  • Watu wengi wanaamini ajali nyingi za machoni hutokana na kazi mbalimbali kama viwandani na maeneo ya ujenzi lakini karibu nusu ya ajali za macho hutokea majumbani tunamoishi.
  • Macho huweza haribiwa kwa kukaa sana juani ukiachana na michezo na kazi nyingine.
  • Kukaa karibu na Tv au Kompuyta kunaweza pelekea kupata maumivu ya kichwa na uchovu wa macho ila haiharibu uwezo wako wa kuona kwani kwa watoto wasioona mbali inabidi wakae karibu.
  • Kuangalia moja kwa moja kwenye jua kunaweza sababisha kuwa kipofu kwa kuharibu sehemu itwayo retina hata kama umevaa miwani zinazopunguza mwanga(nyeusi)
  • Matumizi ya karoti kwa wingi yenye virutubisho vya Vitamin A ni mazuri kwa ajili ya macho lakini Vitamin A haipatikani tu kwenye karoti bali pia kwenye maziwa, mayai na maini.
  • Kuvaa miwani isiyokutosha vizuri haihaiharibu uwezo wa kuona bali miwani yenye lenzi sahihi ndicho kinachohitajika
  • Macho hupungua uwezo wa kuona jinsi umri unavyoongezeka, hapana ukiwa na afya nzuri na kwa kula vyakula vyenye virutubisho, kufanyiwa uchunguzi wa macho na  kutokuvuta sigara utaweza kuwa na uwezo mzuri wa kuona.

“Uwezo wa kuwa na afya nzuri ya macho uko mkononi mwako kwa kuhakikisha msukumo wa damu, kisukari na vyakula vinaendana na afya yako na kusaidia kutunza afya ya macho sasa na baadae”

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show