Kutoboka kwa sehemu ya juu ya jicho (Konea)

Kutoboka kwa sehemu ya juu (mbele) ya jicho ambayo huitwa konea ni jambo ambalo hutokea kwa bahati mbaya. Hali hii ni ya kuogopesha kwani jicho ni sehemu muhimu sana ya binadamu.Hofu nyingi huwa kwenye uwezekano wa kupoteza uwezo wa kuona wa jicho

Japokuwa kuna sababu nyingine ambazo zinaweza kupelekea kutoboka kwa konea, ikiwemo baadhi ya magonjwa yanayoshambulia sehemu ya mbele ya jicho. Ajali imekuwa sababu mojawapo ambayo huwakuta waathirika wengi wa jambo hili. Ajali hizi hutokea katika mazingira yetu ya kawaida tunatoishi kama shuleni na kazini.

Visababishi vya ajali hizi hujumuisha;

  • watoto wanaochezea vijiti kwa kurushiana kama ufagio wa chelewa
  • kufanya kazi (bila kifaa cha kukinga uso) katika mazingira yanayojumuisha kurukiwa na vitu usoni
  • Kupigana kunakojumuisha vitu vyenye ncha

Athari zinazoweza kutokana na kutoboka kwa konea ni pamoja na:

  • sehemu ya ndani ya jicho kusogea kutoka mahali pake pa kawaida na mda mwingine huweza kutoka kwa kupitia kitobo kilichotengezwa
  • damu kujikusanya sehemu ya ndani ya jicho iliyonyuma ya konea
  • lens ya jicho kusogea kutoka mahali pake
  • kupoteza uwezo wa kuona vyema kama mwanzo, na mda mwingine kupoteza kabisa uwezo wa kuona wa jicho lililo athirika

Jambo la muhimu la kufahamu ni kuwa, ajali inayoweza kupelekea kutoboka kwa konea huweza kuzuilika(kujikinga) kwa asilimia kubwa.

“Litunze jicho lako, hifadhi uwezo wako wa kuona” 

1 thought on “Kutoboka kwa sehemu ya juu ya jicho (Konea)

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show