Namna ya kujichunguza matiti.

Uchunguzi wa matiti unaweza kufanywa na mwanamke mwenyewe angalau kila mwezi. Zifuatazo ni hatua rahisi za kufuata wakati wa kujichunguza matiti:

Hatua ya 1:
Simama mbele ya kioo chenye kuweza kuonyesha matiti yote mawili vizuri. Hakikisha upo eneo lenye mwanga wa kutosha. Angalia kama matiti yana uvimbe wowote au mabadiliko katika ngozi kama kuwa na rangi nyekundu au kidonda, angalia pia kubonyea kwa ngozi. Pia angalia chuchu kama zinatoa majimaji au damu, chunguza vidonda vyovyote katika chuchu. Fanya hivi ukiwa umeweka mikono kiunoni, simama kawaida kwa kuweka mikono pembeni ya mwili na kunyanyua mikono juu.

Hatua ya 2:
Nyanyua mkono wako wa kushoto na kwa kutumia vidole vya mkono wa kulia, papasa titi la kushoto kuangalia kama kuna uvimbe wowote. Hakikisha umepitia pande zote za titi. Fanya hivi upande wa kulia wa titi kwa kunyanyua mkono wa kulia na kupapasa titi la kulia kwa mkono wa kushoto.
Unaweza fanya hivi ukiwa bafuni wakati wa kuoga.

 

Hatua ya 3:
Lala chali katika eneo lililonyooka- kama inavyoonekana katika picha. Weka mkono wa kushoto chini ya kichwa ili kukagua titi la kushoto. Baada ya hapo weka mkono wa kulia chini ya kichwa ili kukagua titi la kulia.
Kama utahisi uvimbe wowote katika hatua ya pili au ya tatu, fika kituo cha afya ili kupata vipimo zaidi kutoka kwa wataalamu.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show