Saratani ya matiti

Saratani ya matiti ni saratani itokanayo na ukuaji wa seli za titi bila mpango na usiotokana na mfumo wa kawaida wa ukuaji waseli za mwili.

Saratani hii hutokea kama saratani zingine katika ukuaji wa seli ya saratani kwa kasi kuliko seli za kawaida zamwili.

Takwimu zinaonyesha kuwa nchini Tanzania saratani ya matiti inashika nafasi ya pili kwa kasi ya ukuaji na kuwapata wanawake wengi baada ya saratani ya mlango wa kizazi(cervical cancer) ambayo ni ya kwanza. Na takwimu duniani zinaonyesha kuwa saratani ya matiti ndio inayoongozana hivyo kuonyesha jinsi gani inakuwa tishio sio tu nchini bali kidunia.

Sababu hasa zinazopelekea mtu kupata saratani ya matiti hazijajulikana bado japokuwa baadhi ya tafiti zimeonyesha kuwa mabadiliko ya homoni,mazingira na namna ya maisha huchangia katika kuongeza hatari ya saratani ya matiti kamailivyo kwenye aina zingine za saratani. Pamoja na hiyo kuna vichocheo vinavyofikiriwa kuongeza hatari ya mtu kupatasaratani ya matiti.

Vichocheo hivyo ni vipi hasa?

1. Kuwa mwanamke, hii huongeza hatari ya kupata sarataniya matiti kwani mwanaume wachache sana wanaopatasaratani hii.
2. Mwanamke ambae bado hajazaa
3. Mwanamke mwenye umri mkubwa
4. Mwanamke asiyenyonyesha baada ya kujifungua
5. Historia ya saratani ya matiti katika familia
6. Kupata mimba ya kwanza katika umri mkubwa zaidi yamiaka 30
7. Kurithi vinasaba vinavyongeza hatari ya saratani yamatiti,yaani BRCA1 na BRCA2
8. Kuvunja ungo katika umri mdogo chini ya miaka 12
9. Uzito mkubwa kupita kiasi
10. Unywaji wa pombe
11. Utumiaji wa madawa ya uzazi wa mpango

 

Dalili za saratani ya matiti ni zipi?

-uvimbe kwenye titi usio na maumivu mara nyingi hii ni daliliya awali kabisa.

-mabadiliko ya ukubwa wa titi na muonekano wa titi

-chuchu kutoa majimaji japokuwa mara nyingine zinawezazisitoe

-chuchu kuingia ndani .

-ngozi ya titi kuonekana nyekundu na yenye vishimo vidogo nahivyo ngozi kuonekana kama ganda la chungwa

-mabadiliko kwenye eneo linalozunguka chuchu ,sehemu nyeusiya titi kuonekana kama inayochubuka au kubanduka.

Kumbuka:

Inawezekana kabisa kutibu saratani ya matiti pale inapobainika mapema,hasa katika hatua za mwanzo kabisa ,hivyo ni bora kuzifahamu dalili na kuwahi katika kituo cha afya pale unapoziona kwa uchunguzi zaidi.

2 thoughts on “Saratani ya matiti

 1. Okee,
  [b]Nina swali[/b]
  Je kuna uwezekano wa mtu kupata saratani hizi mbili, moja baada ya nyingine au hata kwa pamoja.

  1. Habari Masha,tunashukuru kwa kutembelea tovuti yetu na kujifunza nasi.
   Inawezekana kabisa mtu akapata saratani hizi kwa pamoja au moja inaanza na baada ya muda mtu anapata nyingine.
   Hii ni kwasababu vitu hatarishi kwa saratani za aina nyingi vinaendana. Na pia saratani huwa na tabia ya kusambaa mwilini pale inapokaa muda mrefu.
   Kama inavyokuwa saratani ya matiti yaweza kupelekea saratani ya mapafu pia!

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show