Je ni sawa mwanaume kuwahi kufika kileleni?

Tatizo la kutofika kileleni kwa wakati ni moja ya matatizo makubwa yanayowakumba watu wengi sana walio katika mahusiano. Wavulana kwa wasichana kwa pamoja wamekua katika janga hila kwa muda mrefu pengine hata kufikia kuyachukia mahusiano waliyonayo kwa sababu ya aibu na kutoridhika.

Kwa kawaida mwanamke na mwanaume wanapaswa kufika kileleni kwa wakati mmoja.
Tatizo la kutofika kileleni kwa wakati kwa wavulana lipo katika pande mbili.

• Kuna wanaowahi kufika kileleni
• Kuna wanaochelewa kufika kileleni(hawafiki kabisa kileleni)

Kutofika kileleni kwa wakati.
Takwimu za tafiti mbalimbali zinaonesha zaidi ya 30% ya wavulana walio katika mahusiano huwahi kufika kileleni kabla ya wakati(premature ejaculation) huku wakiwaacha wenza wao(wanawake) wakiwa bado wanahisia za kuendelea kufanya mapenzi. Kuna sababu nyingi sana zinazolepekea wavulana wengi kuwahi kufika kileleni kabla ya wakati(pre mature ejaculation).
Gusa linki hii kijifunza zaidi sababu zinazopelekea tazizo hili. http://daktarimkononi.com/2018/03/11/tatizo-la-kufika-kileleni-mapema-kwa-wanaume/

Tatizo la kuchelewa (kutofika kabisa) kileleni kwa wakati.
Takwimu za tafiti mbalimbali zinaeleza kua zaidi ya 5-10% ya wanaume walio katika mahusiano hupatwa na tatizo hili la kutofika kileleni. Katika hali hii wasichana hufika kileleni kwa wakati huku wakiwaacha wavulana wakiwa bado hawajafika wisho wa tendo la ndoa. Hali hii huonekana kero kwa wote wasichana na wavulana. Kuna sababu nyingi zinazopeleka hali hii..
• Kuwa muoga wa tendo la ndoa
• Kufikiria matokeo mabaya ya tendo la ndoa wakati wa tendo hilo kama mimba n.k
• Unywaji wa pombe kwa muda mrefu
• Matumizi ya kondomu
• Hasira za muda mrefu
• Kutokua tayari kufanya tendo hili..(kulazimishwa kwa namna yoyote)
• Imani za kitamaduni kua tendo hili ni baya. Hivyo hua na athari kisaikolojia
• Umri mkubwa
• Matumizi ya baadhi ya dawa kama dawa za sonona,na msongo wa mawazo
• Magonjwa mbalimbali kama kiharusi(stroke),kuharibika kwa mishipa ya fahamu ya eneo la siri.
Mambo ya kufanya endapo una matatizo haya (kuwahi kufika kileleni au kutofika kileleni kabisa)
Matatizo haya yanaweza kupungua au kutoweka kabisa kwa kufanya baadhi ya mambo yatakayo kusaidia kisaikolojia na kimwili. Vitu hvyo ni pamoja na.
• Kupunguza au kuacha kabisa matumizi ya pombe au madawa ya kulevya.
• Kutoa imani potofu iliyojengeka juu ya tendo la ndoa
• Kama unatatizo la kuwahi kufika kileleni basi fanya yafuatayo
Tumia kondomu wakati wa tendo la ndoa ili kupunguaza hisia, hii itakusaidia kukaa kwa muda mrefu na pengine kufika kileleni pamoja na mwenzako
 Kua na tabia ya kubadilisha Mkao(style) mara unapohisi unakaribia kufika kileleni, hii itasababisha hisia kurudi na utakua kama unaanza upya.
 Jitahidi kufanya mazoezi ya kuzuia mbegu kwa kuvuta hewa kwa nguvu mara unapohisi unakaribia kufika mwisho, hii itakusaidia kwanza kuanza upya, lakini pia saikolojia yako itahama kutoka mtu wa kumaliza mapema mpaka kuwa bingwa wa mchezo
 Muone mtaalamu wa saikolojia kwa ushauri juu ya magonjwa ya msongo wa mawazo na sonona
 Muone daktari wako ili akupatie dawa za kupaka ili kupunguza hisia na hvyo kukufanya uwe bingwa wa mchezo.
 Fika hospitali kwa vipimo na ushauri zaidi kwani kuna baadhi ya magonjwa husababisha hali hii
 Endapo unaona tatizo lako limekua sugu usiogope kumuona daktari kwani huu pia ni ugonjwa kama magonjwa mengine.
• Fanya mazoezi ili kupunguza uzito na mafuta mwilini.
• Kula mlo kamili, hasa vyakula vya mboga mboga, matunda na mafuta
• Tafiti zinaonesha vyakula vitokavyo kwenye maji chumvi .mfano ngisi na pwezwa husaidia pia

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show