Kufika kileleni (Orgasm) ni kitu gani!?

Kufika kileleni kukiwa kumepewa majina mbalimbali kwa lugha ya kigeni kama “climaxing, coming, orgasm” na mengine mengi; ni hali ya kupata hisia kali za kufurahia kufanya mapenzi wakati wa kufanya tendo hilo. Jinsia zote mbili hupatwa na hali hii.

Nini hutokea wakati wa kufika kileleni!?
Mara nyingi mtu anapofika kileleni mapigo ya moyo hubadilika na kwenda kwa kasi zaidi na upumuaji huwa ni wa haraka na kwa nguvu. Kinachotokea hasa na kusababisha haya hutofautiana baina ya wanawake na wanaume maana maumbile yao ni tofauti pia.

 • Wanawake
  Hali ya kufika kileleni kwa wanawake huambatana na kukaza kwa misuli ya sehemu za siri, kuna baadhi huweza kutoa majimaji yanayorushwa kwa nguvu kutoka kwenye tezi (skene’s glands) zilizo karibu na mrija wa kupitishia mkojo (urethra).

“Endapo mwanamke ataendelea kusisimuliwa kwa wakati huu huweza kufika kileleni mara nyingine tena muda mfupi baada ya ile mara ya kwanza.”

 • Wanaume
  Kwa wanaume hali ya kufika kileleni huambatana na kukaza kwa misuli inayopelekea kutolewa kwa shahawa kwa njia ya kurushwa nje ya uume kwa nguvu. Baada ya hapa hufuatiwa na kusinyaa kwa uume na korodani kitu kinachomfanya mwanaume kupumzika kwa dakika kadhaa mpaka masaa hadi hali ya kufika kileleni ijirudie tena.

Kufika kileleni siyo jambo la furaha peke yake kwani huambatana na faida mbalimbali za kiafya.

7 thoughts on “Kufika kileleni (Orgasm) ni kitu gani!?

    1. Karibu tena Prim
     Kufika kileleni ni hisia inayoanzia kwenye ubongo hivyo basi hata kujihusisha kwenye story zinazohusu ngono (dirty talk) kunaweza kumpeleka mtu afike kileleni, kufanya mapenzi kwa kutumia mdomo pia(oral sex) huweza kumfikisha mwanaume kileleni.
     Punyeto ukiachana na mazuri yake lakini pia Ina madhara yake, moja yaweza kuwa ni utegemezi wa tendo hilo hali inayofanya ushindwe kuridhika pale ukutanapo na mwanamke. Vilevile kufanya punyeto kulikopitiliza hupelekea mtu kuumia na hata kupata maambukizi katika uume maarufu kama “balanitis”

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center