Kwanini sifiki kileleni wakati wa tendo la ndoa?

 

Wanawake wengi hupata ugumu kufika kileleni wakati wa tendo la ndoa. Mara nyingine hutokea hata kama maandalizi yamefanyika vizuri. Hali hii kwa lugha ya kiingereza huitwa “orgasmic dysfunction” . Lakini tufahamu kuwa sio kila anayeshindwa kufika kileleni ana hili tatizo. Zipo sababu ambazo nyingi husababishwa na mahusiano yasiyo mazuri baina ya wapenzi na kupelekea shida hii, ambapo wapenzi wenyewe huweza kutatua matatizo yao na kuweza kuondokana na hali ya kushindwa kufika kileleni.

Nini husababisha ugumu kufika kileleni?

Sababu zinaweza kuwa za kisaikolojia, kimwili, kihisia, kiafya ambazo baadhi zinaweza kuingiliana na za wanaume.

Sababu za kiafya;

 • Magonjwa  kama kisukari na magonjwa mengine yanayosabisha maumivu wakati wa tendo la ndoa ambapo kwa kawaida kama mwanamke anasikia maumivu wakati wa tendo la ndoa hatoweza kufika kileleni.
 • Historia ya upasuaji haswa za wanawake mfano kutolewa kizazi (hysterectomy) . Ambapo kuondolewa kwa kizazi hupunguza kichocheo (testosterone) katika mwili wa mwanamke ambacho husaidia kufika kileleni.
 • Matumizi ya baadhi ya dawa kwa muda mrefu haswa dawa za kupunguza msongo wa mawazo (antidepressants).

Sababu za kisaikolojia;

 • Mtanziko (stress)
 • Msongo wa mawazo
 • Woga wakati wa tendo la ndoa au woga wowote ambao umetawala akili ya mtu.
 • Kukosa kujiamini, aibu
 • Historia ya unyanyasaji wa jinsia mfano kubakwa

Sababu za kimwili

 • Uzee. Jinsi mwanamke umri unavyozidi kuongezeka ndivyo hivyo mwili hupunguza uwezo wa kutengeneza vichocheo vyake (oestrogen) na kupelekea kushindwa kufika kileleni.
 • Uchovu.

Sababu za kihisia

 • Malumbano baina ya wapenzi
 • Kutokuaminiana
 • Kutokuwa na hisia za kimapenzi na mwenza wako.
 • Maandalizi pungufu kabla ya tendo la ndoa.
 • Kutokuridhia kufanya tendo hilo kwa wakati huo.

Nini dalili za “sexual dysfunction”?

 • Dalili kuu ni kushindwa kufika kileleni.
 • Kuchukua muda mrefu sana kupita kiasi kufika kileleni hata kama maandalizi yakiwa ya kutosha.
 • Kutokuridhika kwa kiasi cha ufikaji wa kileleni.

Nini nifanye?

Matibabu yanategemea na sababu ya shida hiyo;

 • Kujitahidi kufanya maandalizi ya kutosha kabla ya tendo la ndoa na mwenza wako.
 • Kupunguza mtanziko (stress), msongo wa mawazo wakati wa tendo la ndoa. Yaani kujitahidi kuweka akili yako yote katika tendo hilo kwa wakati huo.
 • Vilevile kila mmoja kuhakikisha mwenza wake ameridhia kufanya tendo hilo kwa wakati huo na analifurahia.
 • Muone mtaalamu wa saikolojia kwa ajili ya matatizo ya afya ya mahusiano(counseling).Hii itasaidia kusuluhisha matatizo yoyote ambayo mmeshindwa kutatua wenyewe, haya ni pamoja na matatizo yanayowapata wakati wa tendo la ndoa na mengineyo nje ya tendo la ndoa.
 • Tiba ya vichocheo vya mwili ambayo hufahamika kwa Jina la “ oestrogen therapy” ambazo husaidia kuongeza mtiririko wa damu katika sehemu za siri ambapo husaidia mtu kuweza kufika kileleni.
 • Muone daktari kwa shida yoyote ya kiafya kati ya hizo sababu tajwa hapo juu au nyinginezo ambazo unahisi baada ya shida hiyo hali hii imeanza.

3 thoughts on “Kwanini sifiki kileleni wakati wa tendo la ndoa?

 1. Nini maana ya kufikà kileleni kwa mwanamke? Na ni dalili zipi utakazozitumia kujua kuwa mwanamke umemfikisha kileleni wakati wa tendo LA ndoa?

  1. Asante sana Calvin kwa kutembelea tovuti yetu na kujipatia elimu.

   Kufika kieleni kwa mwanamke hakuna tofauti na mwanaume kimaana…ni ile hali ya mwisho kabisa mtu huipatayo wakati wa tendo la ndoa ambayo humpelekea kusema ameridhika (orgasm). Hali hii huambatana na dalili kama vile;
   Misuli ya uke kukaza na kuachia, uke kuloa zaidi, mapigo ya moyo huongezeka kwa kasi, pia unaweza kuona kwa kupitia lugha ya mwili ambapo mwanamke hukusogelea karibu zaidi na kwa nguvu, vilevile wengine hupiga kelele.

   Natumaini nimejibu,endelea kupitia tovuti yetu kwa elimu mbalimbali kila siku
   Asante.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show