malaria kwa watoto

 

Malaria ni moja ya magonjwa hatari ya kuambukizwa yanayoathiri rika zote. Zaidi ya asilimia 50% ya wagonjwa wa malaria duniani hutokea bara la Afrika. Ni moja ya magonjwa yanayohatarisha Maisha katika nchi zinazoendelea kama yasipotibiwa. Vifo zaidi ya milioni moja huripotiwa kila mwaka duniani na wengi wao wakiwa watoto. Watoto waishio katika maeneo ya ukanda wa malaria wapo katika hatari ya kupatwa na Malaria kama hawatakingwa na malaria. Watoto chini ya miaka mitano hupata dalili za hatari za Malaria zaidi kuliko wengine.

USAMBAZAJI WA MALARIA KUTOKA KWA MTU MMOJA KWENDA MWINGINE

Malaria ni ugonjwa wa kuambukizwa unaoenezwa na mbu wa aina ya Anopheles. Mara baada ya kunyonya damu ya mtu anayeugua malaria, mbu huyu hunyonya na vijidudu vinavyosababisha malaria. Mbu huyu anapoenda kunyonya damu ya mtu mwingine huachilia kwenye damu ya mtu huyu vijidudu alivyotoa kwenye damu ya mgonjwa mwingine kwa njia ya kunyonya damu. Mara baada ya vijududu kuingia katika damu ya mtu mwingine husambaa katika chembechembe nyekundu za damu na kuleta dalili za malaria. Mbu anaponyonya damu ya mtu huyu anaweza kusambaza vijidudu vya malaria kwa mwingine kwa njia hiyo hiyo.

DALILI ZA MALARIA KWA MTOTO

Dalili hizi hazitofautiani na mtu mzima isipokua kwa mtoto itaambatana na kulia sana, na kushindwa kunyonya

 • Homa kali
 • Kutokwa na jasho
 • Kuharisha
 • Kutapika
 • Mwili kuwa dhohofu
 • Kichwa kuuma
 • Viungo vya mwili kuuma
 • Kuvimba kwa bandama
 • Kukosa hamu ya kula
 • Kupauka kwa ngozi kuwa ya kahawia
 • Kuishiwa damu

JINSI YA KUJIKINGA NA MALARIA NYUMBANI

 • Tumia chandarua chenye dawa
 • Fukia maji yaliyotuama kuzuia mazingira ya mbu kuzaliana
 • Kata nyasi ndefu kuzuia mazingira ya mbu kuzaliana

Ukiona dalili hizo wahi kituo cha afya na mtoto kwa uchunguzi zaidi kwani malaria isipotibika kwa wakati huweza kuwa sugu na kusababisha kifo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show