Fahamu kuhusu magonjwa ya tezi za mate.

Je unajua kuwa kwa siku moja Tezi za mate hutengeneza mate kufikia kiwango cha lita moja na nusu na kuyasafirisha kupitia mfereji wa mate mpaka katika kinywa chako?

Hii inawezekana kama Tezi tatu kuu zote ambazo huwa mbili mbili katika kinywa cha mwanadamu ni nzima bila kuvamiwa na ugonjwa wowote.

Kitaalamu tezi hizi kuu tatu zinaitwa major salivary glands zilizopo sehemu ya chini ya taya la chini, zingine sehemu ya juu ya mashavu na zingine chini ya ulimi. Tezi hizi kuu zikishirikiana na tezi nyingine ndogondogo nyingi kinywani ziitwazo minor salivary glands kutengeneza mate ambayo yana kazi muhimu katika kinywa mfano mmeng’enyo wa chakula na hata kusaidia kumeza chakula.

Mate huundwa na mchanganyiko wa vitu vingi vya kikemikali ambavyo hufanya mate kuwa kama ute uliotanda juu ya kinywa na kukifanya kinywa kuwa chenye afya kamili.

Magonjwa ya tezi za mate husababishwa na sababu mbalimbali kama zilivyo ainishwa hapa chini, na kila ugonjwa huwa na dalili zake tofauti tofauti na mwingine kutokana na sababu iliyo pelekea ugonjwa huo ingawa maumivu, kinywa kuwa kikavu au kuwa na kiwango kidogo cha mate kinywani pamoja na uvimbe katika maeneo ya tezi za mate ni dalili ambazo huonekana san katika magonjwa mengi.

Zifuatazo ni sababu baadhi ambazo hupelekea Tezi mate kupatwa na shida;

1.Mashambulizi ya bakiteria katika tezi za mate hupelekea ugonjwa kitaalamu huitwa sialadenitis.
2.Kufanyika kwa mawe ndani ya tezi au katika mfereji kitaalamu huitwa sialolithiasis.
3.Saratani ya tezi za mate.
4.Kuzaliwa bila tezi za mate yaani sialoagenesis ambapo mgonjwa huwa na kinywa kikavu.
5.Ajali pia katika eneo la tezi hivyo kupelekea tezi mate kuvimba.
6.Mashambulizi ya Virusi katika tezi ambayo husababisha uvimbe na maumivu makali.

Endelea kutufuatilia daktari mkononi ili upate elimu hii na kuzifahamu dalili mbalimbali za magonjwa tajwa hapo juu na maelekezo yake kuhusu kujikinga na kupata matibabu.

1 thought on “Fahamu kuhusu magonjwa ya tezi za mate.

  1. Mimi nilijibinya maeneo ya tez ya mate kwa sasa naiona imekuwa nzito kama skio linakuwa zito hv….haijavimba wala haiumi sanaaa ni kwa mbali mnoo nahisi uzito je sababu ni hyo kubinya au???maana cjawahi kuhis hyo hali hadi nilivyojibinya

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center