Mawe katika tezi za mate (sialolithiasis)

Mate yanajumuisha vitu mbalimbali kama maji (98%),  madini na kemikali mbalimbali.  Sialolithiasis ni hali ambayo kunakuwa na uwepo wa jiwe au mawe katika tezi za mate. Katika tezi kuu tatu za mate tezi ipatikanayo chini ya taya la chini (submandibular gland)  ndio huathirika zaidi.

Uwepo wa jiwe (mawe) katika tezi husababishwa na vitu mbalimbali ikiwemo

  • Upungufu wa mate, pamoja na kuvunjwavunjwa kwa madini na kemikali mbalimbali zilizopo ndani ya mate kwa sababu ya maambukizi katika koo (oropharyngeal infection ).
  • Uwepo wa maambukizi katika tezi za mate
  • Matumizi ya muda mrefu ya dawa za akili zijulikanazo kama phenothiazines
  • Mara nyingne mawe hutokea bila sababu maalum (idiopathic)

Jiwe linaweza kuwa dogo na kupita katika mirija ya mate na kutolewa mdomoni. Lakini  linapokuwa kubwa hubaki ndani ya tezi au katikati ya mirija na kuziba utolewaji wa mate na mirija hio. Dalili za mtu mwenye jiwe katika tezi za mate ni pamoja na

  • Uvimbe katika sehemu tezi inapopatikana. Uvimbe huu huongezeka zaidi wakati wa kula au mtu anaposikia harufu nzuri ya chakula na mdomo kutoa mate.
  • Uvimbe huu huambatana na maumivu ambayo hutokea zaidi wakati wa kula au mtu anaposikia harufu ya chakula.

Matibabu ya mtu mwenye mawe katika tezi za mate hufanywa na daktari wa kinywa na meno. Mara unapoona uvimbe katika sehemu za  tezi za mate  hakikisha unahudhuria kliniki ya kinywa na meno kwa ushauri,vipimo na matibabu.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show