Dhana potofu kuhusu magonjwa ya akili.

Ugonjwa wa akili ni ugonjwa unaoathiri uwezo wa mtu kufikiri, kudhibiti hisia na tabia.

Kuna dhana nyingi sana kuhusu afya ya akili na wagonjwa wa akili nchini Tanzania. Dhana hizi zinajikita katika vipengele vyote vya magonjwa ya akili yaani sababu zinazosababisha magonjwa ya akili, namna ya kuepuka na hata matibabu. Zifuatazo ni baadhi ya dhana ambazo zipo kwa wingi nchini Tanzania

Je unadhani kuwa magonjwa ya akili yanatokana na uchawi?

-Ukweli ni kwamba magonjwa ya akili huwa kuna yale yanayotokana na mabadiliko ya kibailojia katika ubongo yaani uzalishwaji wa kemikali mbalimbali na mengine hutokana na magonjwa mengine ambapo ugonjwa ukitibiwa na hali ya  akili inarudi kwenye hali yake ya kawaida.

Je ni kweli kwamba magonjwa ya akili yanaambukizwa?

-Hii imani inapelekea watu kuwabagua watu wenye matatizo ya akili kwa sababu watu wanakuwa wanajua kwamba akikaa nae karibu pengine na yeye atapata ugonjwa huo, lakini si kweli hili jambo. Ukweli ni kwamba magonjwa ya akili hayaambukiziki.

Je ni sahihi Kuwabagua,Kuwatenga na kuwapuuza wagonjwa wa akili?

-Hili jambo linatokea sana katika jamii zetu kiasi kwamba watu wanawaita wagonjwa wa akili majina ambayo yanawafanya kujisikia vibaya na kujiona hawana  thamani. Majina kama chizi, hamnazo, punguani na mengine mengi kutegemea na jamii husika. Pia kuwatenga inasababisha kuwaongezea mawazo zaidi wagonjwa na kufanya hali zake kiakili kuchelewa kurudi kwenye hali nzuri.

Kitu kingine ambacho watu hujiuliza sana, Je magonjwa ya akilianatibika?

-Magonjwa ya akili ni kama magonjwa mengine ambayo inambidi mtu atumie dawa katika maisha yake yote kama vile kisukari. Lakini  tofauti ni kwamba kwa upande wa magonjwa ya akili mtu akirudi kwenye akili nzuri huwa wanapewa likizo za dawa ila wanakuwa wanahudhuria kliniki kwa ajili ya uangalizi zaidi.


Magonjwa ya akili ni kama magonjwa mengine tu haitakiwi kuwabagu na kuwapuuza bali tushiriki vyema katika kuwasaidia ndugu na jamaa kuwafikisha hospitali ili wapate matibabu. Pia ni muhimu kuachana na imani za kukimbilia kwa waganga wa jadi.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show