Hakuna mtu kichaa duniani.

Watu wengi kutoka sehemu mbalimbali duniani wamekuwa wakiwaita wagonjwa wa akili vichaa kitu ambacho si sahihi kabisa.Hii hupelekea wagonjwa wa akili kupigwa sana huko mtaani kabla ya kufikishwa katika kituo cha huduma za afya.

Kwani magonjwa ya akili ni nini?.

Huu ni mkusanyiko wa magonjwa ya utimamu wa akili ambayo huathiri uwezo wa kufikiria, furaha, na tabia pia.

Magonjwa ya akili ni kama vile sonona (depression),  wasiwasi uliopita kiasi (anxiety), matatizo ya ulaji na skizofrenia. Magonjwa ya akili yanaweza athiri uwezo wa kufanya kazi za kila siku, masomo kwa wanafunzi, na hata katika mahusiano.

Wagonjwa wengi huwa na dalili ambazo mara nyingi hutibiwa kwa muunganiko wa madawa na tiba ya kisaikolojia.

 

Dalili za magonjwa ya akili ni zipi?

Mara nyingi dalili za magonjwa ya akili hutofautiana kulingana na aina ya ugonjwa, mazingira na sababu ya nyingine. Dalili hizo kwa ujumla zinaweza kuwa kama;

 1. Kujisikia huzuni iliyopita kiasi.
 2. Kuchanganyikiwa au usikivu kupungua sana.
 3. Wasiwasi na woga uliopita kiasi, kuhisi wewe ni mwenye makosa muda wote.
 4. Kuwa na furaha iliyopita kiasi
 5. Kujitenga mbali na marafiki.
 6. Kujisikia uchovu muda wote.
 7. Matatizo ya kukosa usingizi au kulala sana.
 8. Kusikia sauti au kuona vitu ambavyo havipo.
 9. Kutokuwa na uwezo wa kukabiliana na changamoto za maisha.
 10. Kupata na mawazo ya kujitoa uhai
 11. Kushindwa kula kama inavyotakiwa
 12. Matumizi mabovu ya pombe, sigara na madawa ya kulevya.
 13. Magonjwa ya muda mrefu kama kifafa, figo, kisukari na UKIMWI visipothibitiwa ipasavyo.

Wakati mwingine magonjwa ya akili yanaweza kuwa na dalili kama magonjwa mengine ya mwili ambapo mtu anaweza pata maumivu ya kichwa, tumbo , mgongo au maumivu yasiyo na sababu maalum.

Visababishi vya magonjwa ya akili.

Magonjwa ya akili yanaweza sababishwa na sababu mbalimbali za vinasaba na za kimazingira. Sababu hizo zaweza kuwa;

 1. Historia ya magonjwa ya akili katika familia
 2. Changamoto za maisha kama vile ukosefu wa pesa au kumpoteza umpendae.
 3. Matumizi ya pombe na madawa ya kulevya
 4. Kutelekezwa wakati wa utotoni.
 5. Kufanyiwa matendo ya ukatili wakati wa utotoni kama vile kubakwa.
 6. Kupata ajali hasa iliyohusisha kichwa.
 7. Kuwa na marafiki wachache au uhusiano usio salama.
 8. Kushuhudia au kuona jambo la kutisha. Mfano,mabomu ya mbagala.

Matibabu ya magonjwa ya akili.

Endapo utaona dalili tajwa hapo juu au nyingine ambazo zitaashiria uwepo wa magonjwa ya akili unashauriwa kufika au kumpeleka mgonjwa kitup cha afya kilichokaribu kwa msaada na matibabu zaidi.Matibabu yake mara nyingi huwa ni endelevu na anatakiwa kuendelea kutumia dawa kwa kuzingatia masharti ya daktari.

 

Umuhimu wa kuhudhuria kliniki.

Ni vema kwa mgonjwa wa akili kuendelea kuhudhuria kliniki baada ya kutoka wodini kwa kadiri ya maelekezo ya daktari.  Daktari anaweza kumpunguzia au kumuongezea dawa mgonjwa na hata ikibidi kumpa likizo ya dawa kulingana na maendeleo ya mgonjwa.

Cha kuzingatia; Jamii inapaswa kuelewa kuwa watu wenye magonjwa wa akili ni kama wagonjwa wengine wanaosumbuliwa na matatizo mengine katika sehemu mbalimbali za mwili. Hivyo hatupaswi kuwanyanyapaa na kuwatenga bali tuna wajibu wa kuwahudumia na kuwasaidia ili wapone vizuri na kuendelea na majukumu yao ya kila siku.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show