Madhara na jinsi ya kuepuka Trakoma

Mtu akiambukizwa ugonjwa huu mara moja ni rahisi kutibika na antibiotic. Endapo tiba haitafatiliwa, ugonjwa utarudia kumpata mtu mara kwa mara na kusababisha madhara makubwa kwenye macho.

Madhara hayo ni:

1. Vifuniko vya macho vinavimba, nakutengeneza magamba kwa upande wa ndani wa vifuniko.

2. Vifuniko vya macho vinainama kuelekea ndani ya jicho, pia kope zinakua kuelekea ndani ya jicho nakuafanya mkwaruzo kwenye macho.

3. Ukungu unaota kwenye ngozi ya juu ya jicho (ngozi inayofunika duara jeusi la jicho).

4. Mtu anaweza pata upofu kabisa au kutokuona vizuri.

5. Macho yanakua makavu na kuleta hisia ya mchanga kwenye jicho.

Jinsi ya kuepuka/kujikinga na trakoma.

1. Kusafisha uso na mikono mara kwa mara kwa sabuni na maji safi na salama.
2. Tumia maji safi kwa kuoga , kufua na matumizi ya chooni/msalani.
3. Tupa takataka za aina zote sehemu sika na kuweka mazingira safi ili kuzuia uenezaji wa ugonjwa kwa njia ya inzi.
4. Ua inzi kwa dawa za kupuliza.

ZINGATIA USAFI.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show