Athari za uvutaji wa sigara kwenye afya ya kinywa na meno

Watu wengi sana wanafahamu kuhusu madhara ya sigara kwa afya ya sehemu zingine za mwili lakini ni wachache tu wanaofahamu kuhusu madhara ya uvutaji wa sigara kwenye afya ya kinywa na meno kwa ujumla.

Madhara haya ni kama yafuatayo:
• Madoa kwenye meno
• Magonjwa ya fizi
• Saratani ya kinywa
• Harufu mbaya ya kinywa

Madoa kwenye meno
Hali hii husababishwa na moshi utokanao na sigara pamoja na kemikali iliyomo kwenye tumbaku inayoitwa nikotini.Vitu hivi husababisha meno kuwa na madoa ya rangi ya njano na kwa wale ambao wanavuta sigara kwa wingi(heavy smokers),hupelekea meno kuwa na rangi ya kahawia.

madoa kwenye meno

Magonjwa ya fizi
Uvutaji wa sigara hupelekea uzalishaji wa bakteria waharibifu kwenye meno(bacterial plaque) ambao hupelekea magonjwa ya fizi.Pia uvutaji wa sigara husababisha kusinyaa kwa mishipa ya damu iliyoko kwenye fizi na hivyo kupunguza kiwango cha oksijeni kufika katika fizi na hupelekea ulinzi wa fizi kupungua hivyo ni rahisi sana kwa ufizi kuathirika.Magonjwa haya ya fizi hatimaye hupelekea kutokwa na damu kwenye ufizi na meno kulegea.

kuvimba na kutokwa damu kwenye fizi

Saratani ya kinywa na ulimi(carcinoma)
Uvutaji wa sigara kwa mda mrefu huweza kusababisha saratani katika sehemu yoyote ya kinywa.Kitu ambacho watu hawafahamu ni kwamba kila mwaka watu zaidi ya elfu moja wanafariki dunia kwasababu ya saratani hizi

saratani ya ulimi

Harufu mbaya ya kinywa
Hii ni kwasababu ya kuongezeka kwa bakteria waharibifu(plaque) ambao hupelekea mdomo kuwa na harufu mbaya hata pale mvutaji sigara anapopiga mswaki vizuri.

Kwa watu wengi uvutaji wa sigara ni moja kati ya starehe zao japokuwa wanafahamu kuhusu madhara mbalimbali yanayotokana na tabia hii.

Utakapoona dalili zozote za tofauti kwenye meno na kinywa kwa ujumla,ni vyema kumuona daktari wa kinywa na meno kwaajili ya uchunguzi zaidi.

Endelea kutembelea tovuti yetu kujua jinsi ya kupunguza na hata kuacha kuvuta sigara kabisa…..

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show