Ni kwa sababu gani mwanaume huwa tasa/mgumba?

Utasa ni hali ya wanandoa kutofanikiwa kupata mimba au mtoto kwa kipindi cha mwaka mzima ijapokua wanashiriki tendo la ndoa kikamilifu kabisa.

Inakadiriwa zaidi ya 30% ya utasa hutokana na matatizo ya mwanaume, na 10-15% ya utasa hutokana na matatizo ya pande zote mbili(mwanaume na mwanamke).

Kuna sababu nyingi zinazopelekea mwanaume kukosa uwezo wa kutungisha mimba. sababu hizi tunaweza ziweka katika makundi matano tofauti;
i. Matatizo katika uzalishaji wa mbegu za kiume
ii. Kuziba kwa mirija ya kupitishia mbegu
iii. Matatizo ya utoaji mbegu wakati wa tendo la ndoa
iv. Matatizo ya homoni
v. Baadhi ya kemikali zinazozalishwa na mwili huua mbegu za kiume.

1;matatizo ya uzalishaji wa mbegu za kiume
kuna baadhi ya matatizo husababisha kupungua kwa kiwango cha uzalishwaji wa mbegu za kiume au kupelekea kabisa kutozalishwa kwa mbegu;
Matatizo/kasoro ya vinasaba vya mwili.
 Kushindwa kushuka kwa kende za uzazi(korodani) wakati wa ukuaji. Hali hii hupelekea mtu kutoziona korodani kwa nje kama ilivyo kawaida.
 Kuharibika kwa kende za uzazi(korodani) kwa sababu mbalimbali kama ajali, maambukizi na mionzi mikali.
 Baadhi ya dawa na kemikali huchangia pia kuharibu korodani.
 Umri mkubwa, katika umri mkubwa kiwango cha mbegu zinazozalishwa hupungua.
 Unywaji wa pombe kupita kiasi.
 Matumizi ya madawa ya kulevya na uvutaji wa sigara.

2;matatizo katika mirija ya kupitishia mbegu.
Kwa kawaida wakati wa tendo la ndoa mbegu husafiri katika mirija maalumu mpaka kutoka nje, endapo mirija hii itaziba mbegu hazitaweza kutoka nje. Matatizo kama yafuatayo husababishwa kuziba kwa mirija hii.
1; Magonnjwa ya zinaaa ya muda mrefu bila tiba.
2; Magonjwa ya tezi dume
3; Kutokuwepo kabisa kwa mirija hii tokea utotoni
4; Kukatwa kwa mirija hii kama moja yanjia ya uzazi

3;matatizo ya utoaji nje wa mbegu wakati wa tendo la ndoa.
kuna wakati wanaume hupata wakati mgumu kutoa mbegu nje wakati wa kufika kileleni, matatizo haya husababisha mbegu kushindwa kutoka nje hivyo utasa. Matatizo kama;
i.Matatizo ya kufika kileleni hata kabla ya tendo la ndoa
ii. Kushinndwa kabisa kufika kileleni wakati wa tendo la ndoa.
iii. Matatizo katika uti wa mgongo na mfumo wa fahamu kwa ujumla
iv. Baadhi ya dawa na kemikali.
V. Matatizo ya kimaumbile ya uume
vi.Matatizo ya kushindwa kusimamisha uume.

Kwa zaidi ya 80% matatizo ya ugumba na utasa yanatibika katika hospitali na vituo vya afya, ni muhimu kumuona daktari ili kujua nini chanzo cha tatizo lako na kipi kinapaswa kufanyika kwa ajiri ya kutatua tatzo hilo….

1 thought on “Ni kwa sababu gani mwanaume huwa tasa/mgumba?

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show