Utasa (ugumba) kwa wanawake

 

Utasa ni ile hali yakushindwa kupata mimba baada ya kujaribu kupata mimba kwa muda wa mwaka mmoja. Na kwa mwanamke mwenye umri wa miaka 35 ,kujaribu kwa muda wa miezi sita na kuto kupata mimba. Pia mwanamke ambaye anauwezo wa kushika mimba lakini mimba haikai anaweza akawa tasa.

  1. Utasa ni tatizo la wanawake tu?
    Utasa sio tatizo la wanawake tu, utasa ni tatizo la wanawake na wanaume pia. Theluthi ya matatizo ya utasa yanatokana na matatizo ya wanawake, theluthi ya matatizo ya utasa yanasababishwa na matatizo ya mwanaume na theluthi nyingine usababishwa na sababu zisizojulikana au mchanganyiko wa matatizo ya mwanamke na mwanaume.

Nini husababisha utasa kwa mwanamke?
1.Uvimbe kwenye ovari ni tatizo la vichocheo (homoni) kutokuwa sawa na hivyo kuingilia mzunguko wa hedhi na kusababisha yai lisipevuke ipasavyo.

2.Kuziba kwa mirija ya uzazi (fallopian tube)kutokana na magonjwa yanayoshambulia nyonga na mfuko wa uzazi, endometriosis na upasuaji kwenye mfumo wa uzazi.
3.Uvimbe kwenye mfuko wa uzazi.

Vitu ambavyo husababisha hatari kwa mwanamke kupata tatizo la utasa.

1.Umri mkubwa
2.Uvutaji wa sigara
3.Msongo wa mawazo
4.Lishe isiyo bora
5.Kuwa na uzito juu sana au uzito chini sana.
6.Matatizo ya kiafya yanayosababisha kubadirika kwa homoni(vichocheo vya mwili).
7.Magonjwa ya zinaa
8.Mazoezi ya viungo na mbio

Matibabu ya utasa.
Tatizo la utasa linaweza kutibika kwa dawa, upasuaji na upandikizaji wa mbegu za kiume.

3 thoughts on “Utasa (ugumba) kwa wanawake

    1. Asante Ernest kwa swali zuri,kama wote tunavyojua mazoezi ni mazuri na muhimu kwa afya zetu na tunatakiwa kufanya mazoezi mara kwa mara. Mazoezi yanayoweza kupelekea utasa ni yale mazoezi ambayo yanatumia nguvu nyingi kama mazoezi ya wanawake wanariadha,ambapo nguvu nyingi utumika kwenye mazoezi hivyo kusababisha kupungua za mwili zinazoitajika katika kutolewa kwa vichocheo muhimu (homoni) zinazosaidia katika zoezi zima la upatikanaji mimba na mzunguko wa hedhi wa mwanamke.

  1. Asante Ernest kwa swali zuri,kama wote tunavyojua mazoezi ni mazuri na muhimu kwa afya zetu na tunatakiwa kufanya mazoezi mara kwa mara. Mazoezi yanayoweza kupelekea utasa ni yale mazoezi ambayo yanatumia nguvu nyingi kama mazoezi ya wanawake wanariadha,ambapo nguvu nyingi utumika kwenye mazoezi hivyo kusababisha kupungua za mwili zinazoitajika katika kutolewa kwa vichocheo muhimu (homoni) zinazosaidia katika zoezi zima la upatikanaji mimba na mzunguko wa hedhi wa mwanamke.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show