Fahamu visababishi vya homa kwa mtoto mbali na Malaria

Homa ni ongezeko la jotoridi la mwili kwa zaidi ya sentigredi 37. Jotoridi zaidi ya 38.5 ni homa ya kiwango cha juu(high grade fever) ni kiashirio cha maambukizi ya bakteria mwilini. Mbali na bateria, aina nyingine ya vimelea huweza kusababisha homa.Wazazi wengi hufikiria Malaria pekee kama sababu inayopelekea homa kwa mtoto.

 

VISABABISHI VYA HOMA KWA MTOTO

 • Homa ya uti wa mgongo
 • Surua
 • Homa ya matumbo(typhoid)
 • Maambukizi katika njia ya mkojo(UTI)
 • Maambukizi ya sikio kama maambukizi ya sikio la kati(otitis media)
 • Homa ya rhumatiki(rheumatic fever)
 • Kuvimba kwa viungo vya mwili(rheumatoid arthritis)
 • Maambukizi ya kifua kama nimonia, Tb

DALILI ZINAZOWEZA KUAMBATANA NA HOMA NI KAMA;

 • Mtoto kulia kuliko kawaida
 • Kushindwa kula au kunyonya
 • Kupumua kwa haraka
 • Kukohoa
 • Kutokwa na upele
 • Degedege
 • Mwili kukosa nguvu
 • Kushindwa kulala kama ilivyo kawaida kwake

NINI CHA KUFANYA UKIWA NYUMBANI

 • Punguza nguo alizovaa mtoto. Avae nguo nyepesi au asivae kabisa
 • Tumia nguo laini iliyolowekwa kwenye maji vuguvugu kumfuta mtoto ili kuruhusu mvuke kuondoka pamoja na joto mwilini.
 • Mpe mtoto maji ya kutosha au kunyonyesha kwani homa husababisha upungufu wa maji mwilini

Ni vizuri kwa mzazi kuwa na kifaa cha kupimia jotoridi(thermometer) nyumbani ili kuweza kutambua kiasi cha jotoridi kwa mtoto na hivi kumpeleka kituo cha afya mara baada ya kuona limezidi. Muone daktari mapema kwa uchunguzi zaidi kuokoa maisha ya mtoto.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show