Nipake nini kulingana na ngozi yangu

Mara nyingi tumekutana na majina kama “cream” ,”lotion” na “ointment” katika vipodozi au dawa za kupaka tunazonunua kwa matumizi mbalimbali.

Je nini maana halisi ya maneno haya?

Majina haya hutokana na kiasi cha maji na mafuta kilichopo katika bidhaa husika.

Creams: Hizi zina maji asilima hamsini (50%) na mafuta asilimia hamsini(50%). Hii huzifanya cream kupenya kiurahisi kwenye ngozi na kukaa kwa muda mchache kwenye ngozi.

Lotions: Hizi ni kama cream lakini zinakua nyepesi zaidi.

Ointment: Hizi zina maji asilimia ishirini (20%) na mafuta asilimia (80%). Hii huzifanya ointment kutopenya kiurahisi na kukaa muda mwingi kwenye ngozi.

Nitumie nini kulingana na ngozi yangu?

Kuna ngozi aina kuu mbili:
1.Ngozi yenye mafuta mengi
2.Ngozi kavu

Kwa ngozi kavu nashauri matumizi ya bidhaa zilizotengenezwa kama ointment ili kutunza unyevu wa ngozi na kuepuka kubabuka. Kwa matumizi ya kipodozi vaseline inamfaa zaidi mtu mwenye ngozi kavu.
Kwa mtu mwenye ngozi ya mafuta basi bidhaa iliyotengenezwa kama cream au lotion itamfaa zaidi. Hii italeta unyevu kwenye ngozi bila kuongeza mafuta ambayo tayari yapo kwa wingi.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show