Matatizo na magonjwa yatokanayo na kufanya kazi katika sekta ya afya na namna ya kujikinga.

Katika sekta ya afya kuna wafanya kazi katika idara mbalimbali kama vile manesi, madaktari, watu wa radiolojia, wataalam wa maabara, wataalam wa mambo ya mazingira na wafamasia.

Licha ya kazi katika sekta ya afya kuwa ndiyo kazi inayosaidia kuimarisha afya za watu lakini kuna matatizo mbalimbali kiafya ambayo yanaweza kumpata mfanyakazi kutokana na mazingira ya kazi pengine pia kutokana na aina ya matibabu anayofanya.

Matatizo na magonjwa yatokanayo na kada ya afya ni kama yafuatayo;

-Maambukizi mbalimbali ya vimelea kama vile bakteria, fangasi na virusi. Maambukizi haya yanapatikana kwa sababu ya kugusana na mgonjwa bila vifaa vya kinga mf fangasi, kuvuta hewa kutoka kwa mgonjwa mfano kifua kikuu na maambukizi mengine yatokanayo na hewa. Pia kama mtoa huduma ya afya akijichoma sindano iliyotumika kwa mgonjwa mwenye maambukizi ya damu kama vile Virusi Vya Ukimwi (VVU), homa ya ini na mengineyo pia anaweza kupata.

-Kemikali mbalimbali za hospitalini pia zinaathiri afya za wafanyakazi, kwa mfano kemikali za usafi, kemikali za kuhifadhia tishu kwa ajili ya kupima ili zikae muda bila kuharibika.

-Maumivu ya misuli na uchovu kuzidi kiasi kwa sababu ya kubeba wagonjwa wazito na upasuaji unaohitaji nguvu kama vile wa mifupa, pia kusimama muda mrefu wodini na hata kwenye vyumba vya upasuaji.

-Mawazo na huzuni: Mawazo sana yanatokana na kazi kuwa nyingi pamoja na zamu, pia kukaripiwa na wakubwa kazini (bullying) wakati mwingine pia kutukanwa na wagonjwa. Huzuni inatokana na kushuhudia vifo na wakati mwingine mtoa huduma anaweza anza kujilaumu kana kwamba yeye ndo kasababisha kupoteza maisha ya mgonjwa wakati hata siyo hivyo.

-Kwa wanaohudumia wagonjwa wa matatizo ya akili pia inaweza kupelekea kuumizwa kwa kupigwa na wagonjwa ambao wana hasira (violent).

Namna ya kuzuia matatizo haya;

-Kuwapatia chanjo watoa huduma kwa mfano chanjo ya homa ya ini. 37% ya homa ya ini kwa watoa huduma za afya inatokana na kazi hivyo shirika la afya duniani, WHO likaanzisha chanjo hii.

-Kutumia vizuri vifaa vya kujikinga na maambukizi kama mask, gloves, gowns nk.

-Kufuata utaratibu wa matibabu pale inapotokea kujichoma sindano au kitu chochote cha ncha kali ambacho kimetumika kwa mgonjwa. Pia kama damu au majimaji yeyote ambayo yanaweza yakaeneza magonjwa kutoka kwa mgonjwa kwenda kwa mtoa huduma.

-Kuimarisha ulinzi kwenye vituo vya afya sanasana kwenye idara ya magonjwa ya akili.

Licha ya kuwa na changamoto hizi katika kutoa huduma ya afya kikubwa ni kujitahidi kuzingatia namna ya kujikinga (Using protective gears) ili kuendelea kutoa huduma kwa usalama zaidi.

Tunawatakia maadhimisho mema ya siku ya wafanyakazi duniani wafanya kazi wote🙏🙏🙏

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show