Dhana mbalimbali juu ya uvimbe kwenye mfuko wa mayai

Watu wengi husikia ama kuambiwa dhan atofauti juu ya uvimbne katika mfuko wa mayai. Na mara nyingi dhana hizi huwa tofauti au kupishana kidogo na ukweli wa tafiti za kisayansi zilizopo.

Zifuatazo ni baadhi ya dhana kati ya nyingi zinazoaminiwa zikielezewa na ukweli wake wa kisayansi uliopo;

Dhana #1

Uvimbe kwenye mfuko wa mayai huwa ni saratani.

Ukweli ni kwamba, sio kila aina hii ya uvimbe huu huwa saratani na pia ni asilimia ndogo sana huwa saratani au kukua kama saratani

Vilevile uvimbe huu mara nyingi hupotea wenyewe hata bila matibabu na hugundulika katika vipimo vingine mara nyingi bila ya mwanamke kuwa na dalili zozote.

Dhana #2

Uvimbe huu hutokea kwa wenye umri mkubwa tu.

Tafiti zinaonyesha kuwa uvimbe huu hutokea katika rika zote kuanzia mtoto mchanga mpaka umri mkubwa kabisa. Na mara nyingi hukawia kugundulika kwasababu  huwa haina dalili

zozote na hivyo kugundulika katika umri ukiwa mkubwa.

Dhana #3

Uvimbe huu hupelekea ugumba

Hii ni dhana inayofahamika sana na hata kuwatisha wanawake wengi pale wanapogundulika kuwa na uvimbe huu. Uvimbe huu unatibika na mwanamke anaweza kupata ujauzito na sio kama pale mwanamke anapopata endometriosis au uvimbe kwenye sehemu hiyo ya mfuko wa kizazi.

Dhana #4

Uvimbe huu huhitaji upasuaji

Kwasababu mara nyingi uvimbe huu hauna dalili zozote wala hauna madhara kiafya na hata hupotea wenyewe bila hata matibabu.

Na upasuaji huhitajika pale uvimbe unapojirudia mara kwa mara au unapokuwa mkubwa sana.

Dhana #5

Mtu aliyetolewa kizazi hawezi pata uvimbe kwenye mfuko wa mayai

Kizazi kinapotolewa mfuko wa mayai hubaki na hivyo hatari ya mwanamke kupata uvimbe bado ipo.

Dhana #6

Hakuna historia ya uvimbe kwenye mfuko wa mayai hivyo siwezi kupata

Tafiti zinaonyesha kuwa ni asilimia ndogo tu wanawake wanaopata uvimbe huu ndio wenye historia ya uvimbe huu katika familia ,na asilimia kubwa iliyobaki ni wanawake ambao hata hawana historia hiyo.

Uvimbe kwenye mfuko wa mayai huambatana na dalili tofauti pia hupelekea madhara mbalimbali .Ni vyema kutafuta msaada wa kiafya pale unapogundulika kuwa na uvimbe.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show