Maswali na majibu kuhusu busha.

Watu wengi wamekua wakijiuliza maswali mengi sana kuhusiana na ugonjwa wa mabusha, wengi pia wamekua wakipata elimu za uwongo na za kupotosha kuhusiana na ugonjwa huu.

Daktari mkononi ipo kwa ajiri ya kukupa elimu sahihi na majibu ya maswali yako yote ya kiafya. Uliza ujibiwe na madaktari.

Baadhi ya mswali tulio yapokea kuhusina  na ugonjwa huu wa mabusha ni pamoja na.

1; je mabusha husababishwa na kunywa maji ya madafu(nazi)??

Jibu…

“Hapana” mabusha hayahusiani kabisa na unywaji wa maji ya madafu..                                             ugonjwa huu umekua maarufu sana maeneo ya watu wanakunywa maji ya madafu kwa sababu baada ya kunywa maji hayo, Watu hutupa ovyo vile vifuu vya nazi ambavyo baadae huwa mazalia ya mbu wanaoambukiza vimelea vinavyosabasha ugonjwa huu.

2: je ni kwanini ugonjwa huu huwapata sana wakazi wa pwani na visiwani.?? 

Jibu….

Mabusha huwapata sana watu wa pwani na visiwani kwa sababu. Mbu aina ya culex ambae husambaza vilemea aina ya wuchereria bancrofti hupendelea kuishi maeneo ya ukanda wa bahari kulingana na asili yake, hivyo ni rahisi sana kwa wakazi wa maeneo hayo kupata maambukizo ya vimelea hivyo na kupata mabusha.

3:je busha lina madhara gani??

Jibu…

Busha mara nyingi hua halina maumivu.. lakini endapo litapata maambukizi linaweza kusababisha madhara makubwa kama; maumivu ya korodani, hatari ya kupata saratani ya eneo hilo, majipu na hata kuathiri ukuaji wa korodani na kuingilia kazi yake ya kuzalisha mbegu za kiume. Mbali na maambukizi pia mabusha humnyima mtu uhuru wa kutembea endapo litakua kubwa bila kutibiwa. Lakini pia uhuru wa kushiriki tendo la ndoa.

4; je busha linatibika??

Jibu…

“Ndio” busha linatibika kabisa na mtu anapona kabisa na kua kama zamani.. busha linatibiwa kwa hatua mbili. Kwanza kabisa ni dawa za kuua vimelea endapo busha lako ni kwa sababu ya maambukizi…. pili ni upasuaji ambapo maji ya busha huondolewa na kutibika kabisa. Ni bora kuwahi hospitali mapema kabla hali haijawa mbaya.

  • Je swali lako limejibiwa leo?
  • Je una swali lolote kuhusiana na mabusha au ugonjwa wowote??
  • Je una maoni yoyote au ushauli??

Basi kama unaswali lolote au kuna kitu chochote unataka kujua kuhusiana ana afya na magonjwa, tuachie comment yako na sisi tutakujibu.                                               

 

1 thought on “Maswali na majibu kuhusu busha.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show