Fahamu kuhusu tohara kwa watoto wa kike

Tohara kwa wanawake ni tendo la kikatili na lilelatalo maumivu makali, lenye madhara ya kiafya na kisaikolojia

Tendo hili hufanywa kwa kuondoa baadhi ya viungo au viungo vyote vya nje ya uke wa mtoto wa kike kama vile kisimi(clitoris), mashavu ya nje na ndani ya uke (major and minor labias) bila kutumia ganzi wala kuleta usingizi (anaesthesia)

Mara nyingi hufanyika kwa ajili ya mila potofu hasa katika bara letu la Africa na sababu zengine zisizo za kitabibu na hufanywa kwa watoto wa kike walio chini ya miaka 15

Sababu zingine ni kama hutumika kupunguza hamu ya tendo la ndoa kwa mtoto wa kike mpaka atakapoolewa pia wengine huona kama njia ya kumkaribisha mtoto wa kike kuwa mwanamke

Data zilizopo kwa sasa
1)Angalau watoto wa kike 6,000 duniani hufanyiwa tohara kwa siku
2)Mnamo mwaka 2015,watoto wa kike millioni 3.9 walifanyiwa tohara na inatazamiwa namba hii inaweza kuongezeka mpaka milioni 4.6 mwaka 2030 kutokana na ongezeko la watu duniani
3)Nchi nyingi zinazoongoza kwa tohara ni zilizopo Kusini mwa jangwa la Sahara ikifuatiwa na Nchi za Kiarabu na baadhi ya nchi zilizopo Asia,Ulaya na Marekani

Aina za tohara
1)Aina ya kwanza(clitoridectomy)-huhusisha ukataji wa kisimi (clitoris) chote au kidogo
2)Aina ya pili(excision)- huhusisha kutoa kisimi chote au kidogo na shavu la ndani la nje ya uke(labia minora)
3)Aina ya tatu(infibulation)-huhusisha kukata mashavu ya uke na kuziba juu ya uke.hii huleta shida wakati wa hedhi,tendo la ndoa na muda wa kujifungua baadae
4)Aina ya nne-huhusisha njia zisizo za kitabibu kukata,kuchanja sehemu za uke

Madhara ya tohara kwa watoto wa kike

Hutofautianakulingana na aina ya tohara iliyofanyika (Aina ya 3 ya tohara ndo huwa na madhara sana),usafi wakati wa tohara,afya ya mtoto wakati wa tohara,ustadi wa anayefanya tohara

Madhara ya muda mfupi
1)Maumivu makali sana
2)Kutokwa damu kupita kiasi
3)Kupata Tetenasi(tetanus) na maambukizi kutokana na vifaa vinavyotumika kwenye tohara
4)Vidonda na michubuko sehemu za siri
5)Maambukizi ya mfumo wa mkojo (UTI)

Kutokwa na damu kupita kiasi na maambukizi huweza kusababisha kifo kama mtoto hatawaishwa kituo cha afya mapema

Madhara ya muda mrefu
1)Shida wakati wa kujifungua.Wanawake wengi waliokeketwa huhitaji operesheni kujifungua,hutokwa na damu nyingi baaada ya kujifungua pia kutumia muda mrefu kujifungua(prolonged labour)
2)Upungufu wa damu mwilini(Anaemia)
3)Uharibifu kwenye mirija ya mikojo na kuleta shida wakati wa kukojoa(urine incontinence)
4)Maumivu wakati wa tendo la ndoa
5)Kuongezeka kwa uwezekano wa kupata maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kutokana na kisu kimoja kutumika kuchanja watoto wakati wa tohara n.k
6)Madhara ya kisaikolojia mf.sonona,msongo wa mawazo n.k

Nchi nyingi zimeshakataza kwa sheria kuhusu tohara kwa watoto wa kike ikiwemo Tanzania (1998)

Nini cha kufanya
1)Kupata matibabu kutokana na madhara uliyopata kama umewahi fanyiwa tohara mf.kumuona daktari wa maswala ya saikolojia,kufanyiwa upasuaji kuzibua njia ya uke iliyozibwa (deinfibulation) hasa wanaopata shida wakati wa kujifungua/tendo la ndoa

2)Kutoa taarifa kwa vituo husika kwa watoto wa kike walio hatarini kufanyiwa tohara mf.polisi,mashirika yanayohusika na kupinga ukeketaji kama UNICEF,UNDPA n.k

Tendo hili halikubaliki na wote tuna wajibu kulinda na kutetea afya na maisha ya watoto wetu wa kike kwani wao ndo vijana na walezi wa taifa la kesho

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show