Jasho na vipodozi

IMG_E9420

jasho ni nini?

Jasho ni majimaji ambayo hutoka mwilini kupitia matundu madogo yaliyopo katika ngozi.
Mwili hutoa jasho ili kupunguza joto ambalo hupanda katokana na hali ya hewa, homa ama vinywaji vya moto.

Kwanini jasho huwa na harufu hasa kwa mtu aliye balehe?

Harufuย mbaya hutokana na bakteria waliopo kwenye ngozi, ambao hulivunjavunja jasho na kutengeneza ute ambao hutoa harufu. Kuna aina kuu mbili za tezi ambazo hutoa jasho kwenye ngozi:

  1. Eccrine glands-hutoa majimaji na chumvichumvi. Tezi hizi hupatikana sehemu zote za mwili.
  2. Apocrine glands- huanza kufanya kazi baada ya balehe. Tezi hizi hutoa maji maji ambayo husaidia bakteria katika ngozi kushamiri. Tezi hizi zipo makwapani, sehemu za siri na miguuni. Ndio maana sehemu hizo hutoa harufu.

ย  ย  ย  ย  ย  ย  ย  ย  ย  ย  ย  ย  ย  ย  VIPODOZI.

Kutokana na tatizo la jasho na harufu mbaya mwilini, watu hutumia vipodozi mbalimbali kama Perfume, Deodorants, Antiperspirants nk.

DEODORANTS:

Hivi ni vipodozi ambavyo hupunguza harufu mbaya ya jasho kwa kupunguza ukuaji wa bakteria wa kwenye ngozi na pia zina harufu nzuri. Bidhaa hizi hazipunguzi kiasi cha jasho litokalo mwilini.

antiperspirants:

Hizi ni bidhaa ambazo hupunguza kiasi cha jasho litokalo mwilini pamoja na kupunguza harufu. hupunguza kiasi cha jasho kilichopo kwenye ngozi. Humfaa mtu mwenye jasho jingi.ย 

MADHARA YATOKANAYO NA MATUMIZI YA ANTIPERSPIRANTS:

  • Kuziba kwa matundu ya jasho kwenye ngozi, hivyo hupelekea utunzwaji wa uchafu ambao unaweza kua na madhara kiafya.
  • Aleji. vipodozi hivi huwa na kemikali ambazo zinaweza sababisha aleji kwa watu.

Njia asilia ya kuepukana na harufu mbaya ni kwa kuzingatia usafi wa miili na nguo, kutokurudia nguo bila ya kufua nk.

Privacy Preference Center