Korodani kushindwa kushuka chini (cryptochidism)

Utangulizi

Korodani kuto kushuka ni hali ambayo korodani moja au zote mbili hazijashuka kwenye sehemu yake husika (pumbu) .Kutoshuka kwa korodani ni hali ambayo utokea mara nyingi kwa watoto(common) haswa watoto wa kiume waliozaliwa kabla ya umri , ni hali ambayo hinaitaji matibabu .

Sababu za korodani (testicles) kushindwa kushuka chini.

Sababu zinazosababisha korodani kushindwa kushuka chini hazijulikani, ila inasemekana kuwa  inategemea vinasaba, afya ya mama wakati wa ujauzito na mazingira ambapo huweza kuingilia mfumo wa homoni ambao husaidia katika upevukaji wa korodani.

 

Vihatirishi (Risk factors)

  • Kuzaliwa na kiwango kidogo cha uzito
  • Kuzaliwa kabla ya muda (umri wa mimba kutimia)
  • Kuwa na mtu kwenye familia ambaye alikuwa na korodani ambazo hazijashuka.
  • Utumiaji wa pombe na sigara wakati mama ni mjamzito

Wakati gani naweza kumuona daktari?

Kutokuona  korodani kwenye mapumbu sehemu ambayo ilitakiwa kuwepo.Kwa kawaida ikifikia siku za mwisho za ukuaji wa mtoto tumboni korodani huanza kushuka chini na hakizaliwa baada ya miezi  4 korodani inatakiwa ziwe zimeshuka, kwa hiyo baada ya miezi 4  mama asipo ona korodani kwa mtoto anatakiwa amwone daktari. Ili kuwai kutibiwa kwa tatizo hili huepusha madhara ambayo hutokana na hili tatizo.

Je kuna madhara yoyote yatokanayo na tatizo hili?

 Ili korodani zifanye kazi vizuri zinahitaji mazingira yenye baridi  kwa hiyo zisipo shuka chini kwenye pumbu(scrotum) zinakuwa zimeathiriwa na hivyo kusababisha madhara kama ya fuatayo.

1.Matatizo ya uzazi kwa mwanaume ,ambapo mbegu za kiume zinaweza kuzalishwa chache ,kutengenezwa chini ya ubora na kupungua kwa uwezo wa kuzalisha.

2.Huwepo kwenye hatari kubwa ya kupata saratani(kansa) ya korodani.

3.Huweza kupata ngiri

4.Korodani inaweza kuumizwa.