Je nitajuaje nimejeruhi figo zangu ?

Ukisikia au ukisoma nenoย  figo ย nini kinakujia kichwani?

Mwili wa binadamu una figo mbili .

Tuanze na figo kazi yake kuu ni kuchuja uchafu unaokuwepo kwenye damu na uchafu huo kutoka kwa njia ya mkojo.

KUJERUHIWA KWA FIGO

hutokea kwa masaa machache au baada ya siku chache

Inatokea wakati figo inashindwa kuchuja uchafuย  unakuwepo kwenye damu na uchafu huyo ikikaa mwilini inaweza leta ย madhara

ย 

Visababishi vya kujeruhiwa kwa figo kutokana na  sababu kuu tatu ambazo ni

 

Damu kushindwa kufika kwenye figo  kutokana na :

 • Kupoteza damu.
 • Kupotezea kiasi kikubwa cha madini ya sodium na maji mwilini.
 • Moyo kushindwa kufanya kazi.
 • Mshutuko.
 • Ini kushindwa kufanya kazi.
 • Dawa zinaweza kupunguza damu kufika kwenye figo.

Kujeruhiwa kwa figo na

 • Sumu
 • Athari za mzio(allergic reactions )
 • Sepsis
 • Pombe na madawa ya kulevya

Kuzibwa kwa mkojo kutokana na

 • Kuzibwa kwa kibofu cha mkojo (mfano kwa kuvimba kwa tezi dume, kansa ya kibofu cha mkojo)
 • Mawe katika kibofu cha mkojo na mirija ya mkojo

Magonjwa na hali zinaweza sabibisha ni kama vile :

 • Kupoteza damu
 • Dawa
 • Mshutuko wa moyo
 • Magonjwa wa moyo
 • Ini kushindwa kufanya kazi.
 • Kupoteza maji mwilini

Visababishi hatarishi

 • Kulazawa hospitali kama mgonjwa mahututi.
 • Umri wa juu.
 • Kuziba kwa mishipa ya damu miguuni na mkononi.
 • Kisukari
 • Shinikizo la damu
 • Moyo kushindwa kufanya kazi
 • Magonjwa ya figo
 • Magonjwa ya ini

Dalali

 • Kupungua kwa kiwango cha mkojo kinachotoka .
 • Uhifadhi wa maji mwilini ambao hupelekea miguu kuvimba
 • Kukosa pumzi
 • Uchovu
 • Kuchanganyikiwa
 • Kichefuchefu
 • Maumivu ya kifua
 • Kukosa hamu ya kula
 • Kuwashwa

Uatumbuzi kufanyika kwa vipimo vinavyofanyika hospitali

 • Kipimo cha damu
 • Kipimo cha mkojo

Matibabu

 • Kutibu ugonjwa unaosababisha kujeruhiwa kwa figo
 • Kusafisha figo (Dialysis)
 • Kuzuiwa matumizi ya baadhi ya dawa
 • Kula chakula chenye mlo kamili na chenye chumvi kidogo

Privacy Preference Center