Fangasi miguuni

Our about

fangasi ni nini?

Fangasi ni ugonjwa ambao huambukiza na huleta madhara kwenye ngozi ya vidole vya miguuni. Ugonjwa huu hudhuru wana riadha kwa kiasi kikubwa na kupewa jina la ‘Athleteโ€™s foot’ kwa kiingereza.

Fangasi za miguu sio tatizo kubwa ila pia huweza kua shida kutibu tatizo hili. Kwa watu wenye matatizo ya kisukari au wenye mfumo wa kinga ya mwili ambao ni dhaifu na kuhisi kua unapata fangasi, yapasa kumuona daktari mara moja.

Nini husababisha fangasi za miguuni.

Fangasi hutokea pale ambapo vimelea viitwavyo โ€˜tinea fungusโ€™ kukua kwenye miguu. Mtu huweza kupata fangasi moja kwa moja au kwa kua na mawasiliano na sehemu/mtu mwenye fangasi hiyo. Fangasi hushamiri kwneye sehemu za joto na unyevu. Hupatikana hasa kwenye mabafu, sakafu na pia kwenye mabwawa ya kuogelea.

Nani huweza kupata fangasi?

Mtu yeyote huweza kupata fangasi, bali kuna tabia ambazo huweza kuongeza uwezekano wa kupata fangasi. Tabia hizo ni kama:

 • Kutembelea sehemu kama mabwawa ya kuogelea, vyoo vya umma bila ya kuvaa viatu.
 • Kuvaliana soksi, viatu, mataulo na mtu mwenye fangasi.
 • Kuvaa viatu vinavyobana sana.
 • Miguu kukaa na unyevu kwa muda mrefu.
 • Kupata mchubuko katika mguu au vidole alafu kuvaa viatu vya kufunika.

Dalili za fangasi za miguuni:

 • Kuwashwa, kuchoma na kuuma katikati ya vidole au kwenye unyayo wa miguu.
 • Kupata malengelenge kwenye mguu unaowasha.
 • Kupasuka au kutokwa na magamba kwenye unyayo wa miguu.
 • Kua na ngozi mbichi kwenye miguu.
 • Kubadilika ngozi, ugumu na kukatika kwa kucha.

Fangasi huweza kutibiwaje?

Fangasi huweza kutibiwa na dawa zinaptikanazo kwenye maduka ya dawa bila ya kupata kibali kutoka kwa daktari. Dawa za kupaka huweza kusaidia. Pindi zishindwapo kutibu, daktari huweza kukupatia dawa za kunywa na za kupaka na pia kukushauri njia za kuishi ili kuambatana na matibabu. Dawa huweza kua miconazole, terbenafine, clotrimazole, butenafine, tolnaftate, itraconazole nk.

Madhara ya kutokutibu fangasi.

Huweza kusababisha aleji ambazo huweza kupelekea malengelenge na pia kufanya fangasi kujirudia baada ya matibabu.

Jinsi ya kujikinga na fangasi.

 • Kuosha miguu na sabuni na maji kila siku na kuikausha vizuri hasahasa katikati ya vidole.
 • Kupaka dawa ya fangasi kwenye miguu kila siku.
 • Kutokuvaliana soksi, viatu au mataulo na watu.
 • Kuvaa viatu vya wazi kwenye mabafu ya umma, mabwawa ya kuogelea na sehemu zingine za wazi.

Privacy Preference Center