Jinsi gani dawa zinaweza kuharibu au kuathiri figo.

Figo ni ogani muhimu sana mwilini, katika mwili wa binadamu figo ziko mbili kuna figo upande wa kulia na kushoto.

Figo zina kazi zilizo katika makundi yafuatayo; Kazi za kutoa uchafu (uchafu unaozalishwa na mwili, sumu na dawa mbalimbali), Kuweka usawa katika mwili (Kuhakikisha kiwango cha maji, madini na hali ya asidi au alikali mwilini kuwa katika hali stahiki), Kuzalisha homoni ambazo zinasaidia kufanya shinikizo la damu kuwa la kawaida na kubadili vitamin D.
FIGO

Dawa zinaathiri figo kama ifuatavyo;

-Kupunguza damu iendayo kwenye figo; Hali hii inasababishwa na dawa mbalimbali kama vile dawa zinazomfanya mtu kupoteza maji mengi kama vile Lasix. Pia dawa zinazosababisha kupoteza chumvi nyingi, kupunguza kiwango cha damu kinachosukumwa na moyo mfano dawa zinazopunguza shinikizo la damu. Hatimaye figo hukosa damu ya kutosha na kushindwa kuchuja vyema uchafu na kufanya kazi nyingine.

-Dawa nyingine huua seli za figo moja kwa moja. Kwa mfano matumizi ya muda mrefu ya aminoglycosides kama vile gentamycin.

-Pia kuna dawa hufanya njia ya mkojo kuwa nyembamba na kukaza hivyo kuharibu utoaji wa taka kwenye figo matokeo yake figo kuharibika. Kwa mfanoΒ  bromocriptine, methydopa, hydralazine na nyinginezo nyingi.

tulinde figo zetu

Kwa kuwa dawa zinaweza athiri figo zitumiwapo muda mrefu au kwa wingi na pasipo ushauri au uangalizi wa daktari. Hivyo ni vyema kutumia dawa chini ya ushauri na uangalizi wa daktari ili kujiepusha na shida mbalimbali za figo kama vile figo kufeli.


Jagadi Ntugwa MD4 πŸ‡ΉπŸ‡Ώ

#SmartDocπŸ‘–πŸ‘•πŸ‘”βŒšπŸ‘“
mUhAsπŸŽ“πŸ’‰πŸ’Š

All author posts

Privacy Preference Center