Tiba kuu ya figo kushindwa kufanya kazi ni ipi?

Usafishaji na upandikizaji wa figo.

Endapo mgonjwa wa figo ambaye figo yake  imeshindwa kufanya kazi imefika hatua ya mwisho ( End stage renal disease). Mgonjwa akifikia hatua hiyo atalazimika kusafisha figo (dialysis) kila baada ya muda maalum. Lakini tiba iliyo kuu ni kufanyiwa upandikizwaji wa figo (Kidney transplant).

Play Video

Jinsi usafishaji wa figo unavyofanyika

Vigezo gani huangaliwa kabla ya usafishaji.

– Baada ya vipimo vitakavyo onesha kazi ya figo.

-Dalili za mgonjwa 

– Hali ya kiuchumi ya mgonjwa

Nini kinaweza tokea wakati unaendelea kufanyiwa usafishaji?

-Presha  ya mwili inaweza kushuka

-Maumivu ya misuli

-kuwashwa kwa ngozi

-Kupata usingizi kwa shida

-Damu kupungua mwilini.

-Magonjwa ya mifup

-sonona (depression)

 

 

Nini kinatakiwa kufanyika kwa mgonjwa anayefanyiwa usafishaji wa figo.

-Uangalizi juu ya presha na mapigo ya moyo .

       – Mgonjwa anatakiwa kula vyakula kama alivyoshauriwa na daktari.

 

Pia azingatie matumizi ya dawa kama alivyoshauriwa na daktari.

Upandikizaji wa figo ndio tiba kuu kwa mgonjwa ambaye figo yake imeshindwa kufanya kazi kabisa.


Joseph Mwalongo MD5

Saving patients life is my pleasure

All author posts

Privacy Preference Center