Je ni kwanini meno yangu yanalegea?

Meno ya binadamu kwa kawaida yameshikiliwa kwenye mfupa maalumu unaoitwa alveolar bone kwa kutumia nyuzi maalum zinazoitwa periodontal fibres.vyote hivi husaidia meno yetu kuwa imara na kutokulegea.

Inapotokea sasa meno yameanza kulegea meno hayo hushindwa kufanya kazi zake vizuri na hata kuwa kero kwa mhusika kama yamelegea sana.

Sababu mbalimbali zinazopolekea meno kulegea ni kama zifuatazo;

MAGONJWA YA FIZI

   Magonjwa ya fizi ndio yanayoongoza kwa kusababisha meno kulegea  na huanza kwa kuvimba kwa fizi na fizi kutoa damu(gingivitis) ikifuatiwa na ugaga kwenye meno(calculus) na baadae kutokea kwa magonjwa sugu ya fizi(periodontitis).Vyote hivi husababisha mfupa unaoshikilia meno kushambuliwa na kumomonyoka/kulika(alveolar bone resorption) na kufanya meno kulegea.

UVIMBE AU SARATANI KWENYE TAYA

Uvimbe unaohusisha mfupa wa taya usipotibiwa mapema unaweza kuharibu kabisa mfupa wa taya na meno kusababisha meno yaliyopo eneo hilo kulegea na kutoka kabisa.

UJAUZITO

           huweza kusababisha meno kulegea kwa kiasi flani.hii hutokana na mabadiliko ya kifiziologia kwenye mwili wa mama.

AJALI ZINAZOHUSISHA MENO

Ajali zinaweza kusababisha meno kulegea na hata kung’oka kabisa

TATIZO LA KUSAGA MENO (BRUXISM)

Bofya hapa chini ili kusoma zaidi https://daktarimkononi.com/2018/03/04/tatizo-la-kusaga-menobruxism/

KUBAKI NA MENO MACHACHE MDOMONI

Hii hutokana na kung’oa meno mengi na kusababisha meno yaliyobaki kukosa sehemu ya kujishikiza na hivyo kulegea.

ushauri wa kuzingatia

Meno yanapolegea huweza kuambatana na maumivu au yasiwepo kabisa. Sasa watu wengi wanapoona hakuna maumivu hawaoni haja ya kwenda kwa daktari na hivyo hubaki na matatizo haya hadi pale ambapo meno yanaanza kutoka yenyewe.

Ni vizuri kwa watanzania kujijengea tabia ya kufanyiwa uchunguzi wa afya ya kinywa na meno mara kwa mara ili kutunza meno yetu yote.